Vituko ndani ya JF; Upande wangu wa simulizi

Binafsi nilianza kuifahamu Jamii forums tokea enzi ile inaitwa jambo forums, ingawa kwa muda wote huo mpaka kufikia 2012 nilikuwa msomaji tu.

Baada ya kuwa na account rasmi, niliendelea kuangalia mambo mbali mbali yanayojiri JF. Katika kipindi hicho nilifanikiwa kuona mambo mengi tu mengine ya kufarahisha, kuhuzunisha pia na kuelimisha.

Kwa kiasi kikubwa nimepata elimu kubwa sana juu ya tabia halisi za watanzania kwa ujumla, ukifuatilia mtandao huu, utaweza kusoma mind za watu mbali mbali kwakua wanauhuru mkubwa wa kufanya hivyo nyuma ya utambulisho usio halisi tofauti na matumizi ya utambulisho halisi.

Kwa ufupi tu haya ni baadhi ya mambo niliyobahatika kuyaona humu kutokana na kuwa member wa jukwaa hili;

UMILIKI WA ID (Utambulisho) ZAIDI YA MMOJA:
Sheria za jukwaa zinamtaka kila anayetaka kuanzisha au kuchangia mada yoyote awe amejiandikisha na kuwa mwanachama wa jukwaa hili.

Baada ya kujiandikisha mhusika hutambulika kwa jina alilochagua yeye kama utambulisho wake, ingawa ni makosa vile vile kuwa na utambulisho zaidi ya mmoja.

Kutokana na hitaji hilo kuwa la lazima, baadhi ya wanachama wameamua kutumia vibaya nafasi hiyo kwa kumiliki zaidi ya ID moja.

KUANZISHA MADA NA KUICHANGIA MWENYEWE:
Kuna baadhi ya wanachama lakini sio wengi huamua kuanzisha mada na kutumia ID nyingine za akiba kujibu mada aliyoianzisha mwenyewe.

Aina hii ya wanachama ni wale wanaotaka kuvutia wingi wa comments katika mada zao wanazozianzisha. Ingawa bado haijajulikana nini malengo yao halisi lakini swala la kuanzisha mada na kuichangia mwenyewe kwa ID nyingine za akiba lipo sana.

KUANZISHA MADA NA KUJISIFIA KWA ID YA AKIBA.
Kuna baadhi ya wanachama hupenda kuanzisha mada na kujisifia mwenyewe kwa kutumia ID ya akiba.

Utakuta mwanachama anaandika Mada halafu kwa kutumia ID nyingine hutoa comment ya kujisifia mfano mzuri huwa katika kauli kama hizi. " Aisee wewe jamaa nakukubali, unaakili sana".

WANAUME KUMILIKI ID ZA KIKE.
Kuna baadhi ya ID zenye majina ya kike, wamiliki wake ni wanaume kabisa.
Ingawa haijajulikana nini malengo yake halisi, ila unakuta michango ya wahusika wakitumia ID hizo za kike zinatoa viashiria vingi sana kuwa mmiliki wa ID hiyo sio wanamke halisi.

WATU MAARUFU KWA KILA JUKWAA.
Jamiiforums , katika kujiimarisha imeweka majukwaa mbali mbali ili kuwezesha mijadala iweze kuwa katika mpangilio. Ni katika mpangilio huo huo, kumezuka baadhi ya watu kuwa maarufu ama wakongwe katika jukwaa.

Watu hawa wanaushawishi mkubwa na maamuzi pia katika michango. Hivyo kama ni mgeni ni vyema ukawa makini kujifunza kupitia wakongwe wa kila jukwaa.

WATU MAARUFU KWA UJUMLA.
Kuna baadhi ya members kutokana na ukongwe na michango yao katika jamii forums wamebahatika kukubalika katika kila jukwaa.
Hawa wakienda jukwaa lolote bado mada zao hupata wachangiaji wengi tu.

KUMILIKI ID ZA PANDE KINZANI. ( CCM Vs UKAWA).
Kuna baadhi ya members humuliki ID zinazowakilisha hoja kinzani kwa malengo maalum. Utakuta member fulani anamiliki ID inayosifia CCM na wakati huo huo inayoikashifu CCM. Atamiliki ID inayosifia Chadema na inayoikashifu Chadema.

Hawa ni wataalam kabisa ambao bila kuwa makini hutaweza kutambua kama ni yule yule anayemiliki ID mbali mbali hapa jamvini.

Wadau kwa ufupi ni hayo tu. Ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu hapa jamvini. Naweza kuwa sahihi au sio sahihi.
Hata mimi mkuu tangu nijiunge humu leo ndo nimeona uzi wako maana hua naonaga tuu coment zako
 
Na hiki kingine mtoa mada anatoa mada alafu zinakuja team ma mdogo, mpwa, mjomba yaani hamna mambo ya kujenga ni umbea umbea

Wengine wakiona id za kike ndo ashapata mteremko alafu ni memba wakongwe ila wanakuwa wavulana waliobalehe jana.

Hongereni wanao tendea haki id zao na ukongwe wao
Asante mkuu kwa kunisemea duku duku langu
 
Binafsi nina mpango wakufungua id ya pili kwa ajili ya jukwaa la siasa maana kwa hali ilivyo unaeza shangaa unaenda pimwa mkojo kwa ajili ya id yako ambayo umeisajili na kuweka utambulisho wako wa kweli japo user name ni fake
 
Nlikuwa sjaangalia aliyeanzisha mada ni nani

Kumbe ni stroke.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Deogratius Kisandu unamuweka wapi hapo? (Nadhani sijakosea jina lake asije kuniingiza kwenye list ya watu wa kuwashtaki)
 
Binafsi nilianza kuifahamu Jamii forums tokea enzi ile inaitwa jambo forums, ingawa kwa muda wote huo mpaka kufikia 2012 nilikuwa msomaji tu.

Baada ya kuwa na account rasmi, niliendelea kuangalia mambo mbali mbali yanayojiri JF. Katika kipindi hicho nilifanikiwa kuona mambo mengi tu mengine ya kufarahisha, kuhuzunisha pia na kuelimisha.

Kwa kiasi kikubwa nimepata elimu kubwa sana juu ya tabia halisi za watanzania kwa ujumla, ukifuatilia mtandao huu, utaweza kusoma mind za watu mbali mbali kwakua wanauhuru mkubwa wa kufanya hivyo nyuma ya utambulisho usio halisi tofauti na matumizi ya utambulisho halisi.

Kwa ufupi tu haya ni baadhi ya mambo niliyobahatika kuyaona humu kutokana na kuwa member wa jukwaa hili;

UMILIKI WA ID (Utambulisho) ZAIDI YA MMOJA:
Sheria za jukwaa zinamtaka kila anayetaka kuanzisha au kuchangia mada yoyote awe amejiandikisha na kuwa mwanachama wa jukwaa hili.

Baada ya kujiandikisha mhusika hutambulika kwa jina alilochagua yeye kama utambulisho wake, ingawa ni makosa vile vile kuwa na utambulisho zaidi ya mmoja.

Kutokana na hitaji hilo kuwa la lazima, baadhi ya wanachama wameamua kutumia vibaya nafasi hiyo kwa kumiliki zaidi ya ID moja.

KUANZISHA MADA NA KUICHANGIA MWENYEWE:
Kuna baadhi ya wanachama lakini sio wengi huamua kuanzisha mada na kutumia ID nyingine za akiba kujibu mada aliyoianzisha mwenyewe.

Aina hii ya wanachama ni wale wanaotaka kuvutia wingi wa comments katika mada zao wanazozianzisha. Ingawa bado haijajulikana nini malengo yao halisi lakini swala la kuanzisha mada na kuichangia mwenyewe kwa ID nyingine za akiba lipo sana.

KUANZISHA MADA NA KUJISIFIA KWA ID YA AKIBA.
Kuna baadhi ya wanachama hupenda kuanzisha mada na kujisifia mwenyewe kwa kutumia ID ya akiba.

Utakuta mwanachama anaandika Mada halafu kwa kutumia ID nyingine hutoa comment ya kujisifia mfano mzuri huwa katika kauli kama hizi. " Aisee wewe jamaa nakukubali, unaakili sana".

WANAUME KUMILIKI ID ZA KIKE.
Kuna baadhi ya ID zenye majina ya kike, wamiliki wake ni wanaume kabisa.
Ingawa haijajulikana nini malengo yake halisi, ila unakuta michango ya wahusika wakitumia ID hizo za kike zinatoa viashiria vingi sana kuwa mmiliki wa ID hiyo sio wanamke halisi.

WATU MAARUFU KWA KILA JUKWAA.
Jamiiforums , katika kujiimarisha imeweka majukwaa mbali mbali ili kuwezesha mijadala iweze kuwa katika mpangilio. Ni katika mpangilio huo huo, kumezuka baadhi ya watu kuwa maarufu ama wakongwe katika jukwaa.

Watu hawa wanaushawishi mkubwa na maamuzi pia katika michango. Hivyo kama ni mgeni ni vyema ukawa makini kujifunza kupitia wakongwe wa kila jukwaa.

WATU MAARUFU KWA UJUMLA.
Kuna baadhi ya members kutokana na ukongwe na michango yao katika jamii forums wamebahatika kukubalika katika kila jukwaa.
Hawa wakienda jukwaa lolote bado mada zao hupata wachangiaji wengi tu.

KUMILIKI ID ZA PANDE KINZANI. ( CCM Vs UKAWA).
Kuna baadhi ya members humuliki ID zinazowakilisha hoja kinzani kwa malengo maalum. Utakuta member fulani anamiliki ID inayosifia CCM na wakati huo huo inayoikashifu CCM. Atamiliki ID inayosifia Chadema na inayoikashifu Chadema.

Hawa ni wataalam kabisa ambao bila kuwa makini hutaweza kutambua kama ni yule yule anayemiliki ID mbali mbali hapa jamvini.

Wadau kwa ufupi ni hayo tu. Ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu hapa jamvini. Naweza kuwa sahihi au sio sahihi.
Aisee wewe jamaa nakukubali, una akili sana.

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Hapana, huyu ni Mkenya anaitwa nikk mutuma ingia Google utamjua vizuri
e72c5102c9f83176918b0cf637383363.jpg

d1e84ac25622e9c783ae381fc2e8e52f.jpg

5ddbfb4bfc523712689d394ca4272481.jpg
314fc650201194d5cc8c86cd8e12d962.jpg
3fe73ad6a04a321fa3c2fde557132dc9.jpg
3c7231b595ec70032d303da8f5730499.jpg
aeb47141c3b915c580f50c383a6ff482.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
we jamaa nakukubali duh! umepost mulemule nilichotaka kupost 🙂
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom