Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 38,610
- 49,009
Binafsi nilianza kuifahamu Jamii forums tokea enzi ile inaitwa jambo forums, ingawa kwa muda wote huo mpaka kufikia 2012 nilikuwa msomaji tu.
Baada ya kuwa na account rasmi, niliendelea kuangalia mambo mbali mbali yanayojiri JF. Katika kipindi hicho nilifanikiwa kuona mambo mengi tu mengine ya kufarahisha, kuhuzunisha pia na kuelimisha.
Kwa kiasi kikubwa nimepata elimu kubwa sana juu ya tabia halisi za watanzania kwa ujumla, ukifuatilia mtandao huu, utaweza kusoma mind za watu mbali mbali kwakua wanauhuru mkubwa wa kufanya hivyo nyuma ya utambulisho usio halisi tofauti na matumizi ya utambulisho halisi.
Kwa ufupi tu haya ni baadhi ya mambo niliyobahatika kuyaona humu kutokana na kuwa member wa jukwaa hili;
UMILIKI WA ID (Utambulisho) ZAIDI YA MMOJA:
Sheria za jukwaa zinamtaka kila anayetaka kuanzisha au kuchangia mada yoyote awe amejiandikisha na kuwa mwanachama wa jukwaa hili.
Baada ya kujiandikisha mhusika hutambulika kwa jina alilochagua yeye kama utambulisho wake, ingawa ni makosa vile vile kuwa na utambulisho zaidi ya mmoja.
Kutokana na hitaji hilo kuwa la lazima, baadhi ya wanachama wameamua kutumia vibaya nafasi hiyo kwa kumiliki zaidi ya ID moja.
KUANZISHA MADA NA KUICHANGIA MWENYEWE:
Kuna baadhi ya wanachama lakini sio wengi huamua kuanzisha mada na kutumia ID nyingine za akiba kujibu mada aliyoianzisha mwenyewe.
Aina hii ya wanachama ni wale wanaotaka kuvutia wingi wa comments katika mada zao wanazozianzisha. Ingawa bado haijajulikana nini malengo yao halisi lakini swala la kuanzisha mada na kuichangia mwenyewe kwa ID nyingine za akiba lipo sana.
KUANZISHA MADA NA KUJISIFIA KWA ID YA AKIBA.
Kuna baadhi ya wanachama hupenda kuanzisha mada na kujisifia mwenyewe kwa kutumia ID ya akiba.
Utakuta mwanachama anaandika Mada halafu kwa kutumia ID nyingine hutoa comment ya kujisifia mfano mzuri huwa katika kauli kama hizi. " Aisee wewe jamaa nakukubali, unaakili sana".
WANAUME KUMILIKI ID ZA KIKE.
Kuna baadhi ya ID zenye majina ya kike, wamiliki wake ni wanaume kabisa.
Ingawa haijajulikana nini malengo yake halisi, ila unakuta michango ya wahusika wakitumia ID hizo za kike zinatoa viashiria vingi sana kuwa mmiliki wa ID hiyo sio wanamke halisi.
WATU MAARUFU KWA KILA JUKWAA.
Jamiiforums , katika kujiimarisha imeweka majukwaa mbali mbali ili kuwezesha mijadala iweze kuwa katika mpangilio. Ni katika mpangilio huo huo, kumezuka baadhi ya watu kuwa maarufu ama wakongwe katika jukwaa.
Watu hawa wanaushawishi mkubwa na maamuzi pia katika michango. Hivyo kama ni mgeni ni vyema ukawa makini kujifunza kupitia wakongwe wa kila jukwaa.
WATU MAARUFU KWA UJUMLA.
Kuna baadhi ya members kutokana na ukongwe na michango yao katika jamii forums wamebahatika kukubalika katika kila jukwaa.
Hawa wakienda jukwaa lolote bado mada zao hupata wachangiaji wengi tu.
KUMILIKI ID ZA PANDE KINZANI. ( CCM Vs UKAWA).
Kuna baadhi ya members humuliki ID zinazowakilisha hoja kinzani kwa malengo maalum. Utakuta member fulani anamiliki ID inayosifia CCM na wakati huo huo inayoikashifu CCM. Atamiliki ID inayosifia Chadema na inayoikashifu Chadema.
Hawa ni wataalam kabisa ambao bila kuwa makini hutaweza kutambua kama ni yule yule anayemiliki ID mbali mbali hapa jamvini.
Wadau kwa ufupi ni hayo tu. Ni mtazamo wangu kutokana na uzoefu wangu hapa jamvini. Naweza kuwa sahihi au sio sahihi.