Pamoja na huduma mbovu za baadhi ya wafanyakazi wa benki labda wateja wengine nao wana matatizo. Au wengine mnaenda benki tofauti kila siku?
Benki yako(yaani una akaunti hapo muda mrefu) lazima utakuwa unajulikana na wahudumu wengi tu na mnaweza kuwa marafiki kitu ambacho kitakusaidia kupata huduma nzuri ambayo unastahili kuipata hata ukiwa huna rafiki.
Mimi ninapo-bank nawajua wahudumu wote hadi branch manager kwa sababu hii labda ndio maana napata first class service,wafanyakazi wote wa bank hadi walinzi wa security company wananifahamu na ni 'marafiki'
Habari ya kuibiwa hela na teller ukishafahamiana na hawa watu haipo,tena muda mwingine unakuta foleni kubwa au system down unamuachia hela anakugongea tu muhuri system ikiwa fresh anamalizia transaction.
Tuwaheshimu wengine na sisi watatuheshimu.