kocha Nabi
JF-Expert Member
- Feb 1, 2022
- 600
- 1,513
karibu tufurahishane, na kushare visa mbalimbali ambavyo umewahi kukutana navyo ukiwa safarini.
kuna siku nilipanda basi(kilimanjaro exp) tanga (kabuku) ikitokea arusha to dar mida ya saa3 usiku wakati tumeiacha msata maeneo ya mwetemo tukiwa tunaitafuta kiwangwa, basi ilipata hitirafu na kuzima katikati ya bara bara
kimbembe kilikuwa mlango umegoma kufunguka coz mifumo yote haifanyi kazi. wenye uwezo tulitokea dirishani na kuwahi kuweka majani kwani hata triangle gari haikuwa nayo, ndani ya basi kulijaa moshi tukawa tunasaidia watu kitoka dirishani kumbuka basi ni refu ukiwa unatokea kwa dirishani. na ilikiwa ukitolewa lazima watu wakumulike na torch za simu ili wakuelekeze pa kukanyaga hatimaye wakusaidie.
hii siku wanawake waliovaa sketi bila kukali walifunua nguo zao ili wapate kutoka kwani ndani ilikuwa kila mtu anaokoa roho yake.
baada ya zoezi kukamilika ndipo balaa kamili lilianza, nakumbuka ilikuwa mida ya saa 6 usiku wakati tunasubiri gari nyingine kutubeba, kuna semi ya mafuta ilikuwa full ikitokea msata uelekeo bagamoyo, speed iliyokuwa nayo ni kama ndege inataka kufanya takeoff.
kuja kutahamaki mbele kuna gari ambayo haiwaki taa ya aina yoyote kulia pia kuna gari inakuja. alichoamua ni kuelekeza upande wake wa kishoto ambao watu walijilalia kwenye majani wenye kuwasiliana na ndugu, wenye kupiha dua, wenye kulala n.k.
mimi kwa uelewa wangu wa majanga nililicha gari mita 100 nikakaa zangu nikimsoma mwanagu rikyboy na uzi wake pendwa. gjafla nkaona kundi la watu likitimka mwenye kuingia kichakani, mwenye kutaka kurudi kwenye gari, mwenye kuingia chini ya uvungu kila mmoja alikuwa na uelekeo wake.
hakika lilikuwa tukio la kuhuzunisha ila kwa rehema za Mungu dereva alijitahidi kusimamisha gari hadi tank ilipakaa mafuta tu yakimwagika kwa kunesa.
nina hakika humu tumekutana sana na vituko tukiwa safarini, karibu ushare nasi tujifunze.