Hivi kwanini marehemu wanafungwa hivi....?
Najua ni sanda... ila....
Kaka yangu mmoja alifia nyumbani, nikiwepo na nilikuwa na wakubwa zangu (wazazi). Mmoja wa wazazi nikiwa nae, nilijikaza na sijui zile nguvu zilitoka wapi....
Ilikuwa usiku, kwanza akili ilikataa kuwa ameshafariki maana bado alikuwa wamoto. Nakumbuka nilikuwa na huyo mkubwa wangu kuandaa mwili kutoka nyumbani kwenda mochwari....
Sitasahau usiku ule....
Mkubwa wangu akaniambia tumvue nguo zote wataziiba kule mochwari, sikumuelewa... wataibaje nguo za mgonjwa hata kama hajitambui? Mimi ntakaa nae kumlinda wasimuibie... akili haikukubali kabisa kuwa anaenda kulala mochwari hadi taratibu za mazishi zikamilike.....
Sitasahau asilani, nakumbuka nilikataa na nikamgomea mkubwa wangu tumfunge na shuka na kufunga na kamba.....
Ilikuwa ndo mara ya kwanza nashuhudia ndugu wa karibu amenifia, kuandaa mwili, alikuwa bado wamoto akaanza kupoa kutokea miguuni hadi kichwani.....
Asieeeh..... Acha tuu.... hadi hisia zimenirudia.....
Wakati anatoa pumzi yake ya mwisho nilimsikia, daaah..... kifo hakina huruma....
Ni siri na fumbo kubwa sana hakuna mwanadamu aliyefanikiwa kulitatua.
Ule msiba nilikondaa.... ila nilikonda na mengi....
Ni kaka aliyeniachia kumbukumbu mujarabu nyingi sana....
Alikuwa mkubwa sana kwangu, wakati naanza shule ya awali ndo alikuwa akinipeleka kisha anaenda shule yake (shule zilikuwa karibu).
Wakati naripoti chuo kikuu,siku ya kwanza alinipeleka chuo na gari yake, miaka hiyo....
Tabia zetu ziliendana, tulishirikishana mambo mengi, he was my partner in crime...
Alinionya mambo mengi ambayo hayapasi binti kufanya, somehow was like a father (by then mshua bize na mambo ya sirikali). Alinifunza ujasiri wa kiume pia, michezo yangu ya utotoni hadi binti mingi Ilikuwa ya kiume. Shida Ilikuwa geti kali na juu nina makaka tuu na chini makaka, wakike hadi mabinamu waje likizo hiyo....
Nilimsikiliza kaka yangu, nilimtii na nilimpenda sana, nae alijua nikimwambia kitu Kasie atanifanyia... mara kibao nilimfulia nguo zake, nilimuandalia chakula...
Ooh, tears shed my eyes...
What a memory today, he was such a soul....
Sijui ndo ile wanasema kizuri hakidumu....🤔🤔🤔🤔
Hakufikisha hata miaka 40....
Nakumbuka katikati ya msiba kabla hatujazika, kuna usiku niliota akatokea akaniambia sister usijali, kuna kitu flani aliniambia kikaja kuwa kweli....
Hadi milele sitokaa nipoteze kumbukumbu ya huyu kaka yangu.
Laiti angekuwa hai hadi leo, mambo mengi yaliyonitukia yasingekuwa kama yalivyotokea...
Where you are bro, I smile back 🥲.