Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,582
- 1,105,378
Baadaye wakuu. Mungu na Akatubariki sote. Asanteni kwa burudani na vicheko 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
mpumzishe sasa akale matikiti😅Napenda kkuona unavyo teseka![]()
😅😅 Naipenda sana face ya Anna tumefanana Kwa mbaliiNitafurahi mno...
Sasa umeweka ya Anna dah!
By the way, kimalaika chako kina miezi mingapi sasa? Kimeanza kusimama? 😁😁😁🏃🏿♂️
Daaah, kweli bongo mpaka tutoboe Yesu atakuwa amerudiNimecheka sana leo. Ameandika rafiki yangu Yuda Madai
MTU mmoja alifariki na kwenda jehanamu. Kufika huko akakuta kuna jehanamu tofauti tofauti kwa kila nchi. Akaamua kuzunguka zunguka ili aweze kuipata jehanamu yenye maumivu kidogo zaidi.
Akaiendea jehanamu ya Ujerumani. Akamwuliza mtu aliyemkuta mlangoni. "Wanakufanyaje ukiingia humu?"
Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kijerumani anakucharaza bakora kutwa nzima."
Mtu huyo hakuipenda kabisa jehanamu hiyo. Akaamua kujaribu jehanamu za Marekani, Uingereza, Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini akagundua kuwa zote zina adhabu sawa tu na jehanamu ya Ujerumani.
Kisha akaifikia jehanamu ya Tanzania. Akastaajabu kuona kuna foleni ndefu kweli ya watu wakisubiri kuingia humo. Kwa mshangao usiosemekana akauliza, "Jamani kwani humu wanawafanyaje?"
Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kitanzania anakucharaza bakora kutwa nzima."
Akazidi kustaajabu. Akauliza, "Lakini mbona kinachofanyika humu ni sawa kabisa na kinachofanyika kwenye jehanamu zingine, sasa kwa nini hapa kuna foleni kubwa sana watu wote wanakimbilia huku?"
Jamaa mmoja akamshika mkono. Akamvutia pembeni. Akamnong'oneza, "Watu wanakimbilia huku kwa kuwa jehanamu ya Tanzania haina umeme wa uhakika, unakatika katika kila dakika kwa hiyo kiti cha umeme hakifanyi kazi. Halafu pia misumari ilishalipiwa lakini wala haijaletwa na mzabuni kwa hiyo kitanda cha humu ni raha tu kukilalia. Na jambo jingine ni kuwa shetani wa Kitanzania alipokuwa duniani alikuwa mtumishi wa umma. Kwa hiyo ameshazowea kufika ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio na kisha kuondoka zake kwenda kufanya shughuli zake binafsi."halafu mkaguzi wa Kitanzania CAG hana meno yeyote hawezi kufanya chochote kumuwajibisha Shetani ndio maana foleni ni kubwa hata yule shetani mwingine anayeshughulikia mawasiliano pia yeye hajui kutumia vyombo vya kiteknolojia hivyo hajui hata tofauti ya internet na mtandao kwa kifupi jehanamu ya Kitanzania ni full bata unaenjoy hakuna ufuatiliaji wowote hata shetani ameweka ndugu zake huwa mara ingine wanakata umeme ili wauze majenereta hivyo jehanamu ya Tanganyika ni fake haina ukwelie tu.
Note: fasihi iliyotumika hapa inatosha kutoa taswira namna wananchi wanavyoiona nchi yao.
😂😂😂😂😂na mimi pia naunga andamano
Mimi mara ya mwisho kuwa na wivu wa kuchapiwa ni 2012, nilipigiwa kisura changu kipindi hicho nikiwa naona!Hela hazihusiani na kuchapiwa...ila unazihitaji ili kuimenteini pisi kali kama hii. Kuna msemo kuwa eti pisi kali huwa hazili matembele hasa zikiwa kwenye peak sijui kama ni kweli...
Uwe na hela usiwe nazo kuchapiwa kuko pale pale tu
View attachment 2809437