#HABARI Katika hali isiyo ya kawaida mwili wa kijana Idd Salum anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22, uliozikwa jana Jumatano Oktoba 11, 2023, katika makaburi ya Waislam mtaa wa Nyahingi kata ya Mkolani jijini Mwanza umekutwa umefukuliwa na watu wasiojulikana na kuondoka na sanda ya marehemu.
Kwa mujibu wa kiongozi katika msikiti wa Khayrudini Mkolani Said Mselem, amesema walifika asubuhi kwa ajili ya swala na kukuta hali hiyo, na kuongeza kuwa huenda waliofanya tukio hilo waliruka ukuta wa fensi ya makaburini hapo, kisha kufukua kaburi hilo na kuondoka na sanda ya marehemu.
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefika katika eneo la tukio na baada ya uchunguzi wa awali limeruhusu mwili huo uzikwe tena.
#EastAfricaRadio
View attachment 2780207
Sent using
Jamii Forums mobile app