

Mchungaji Prosper(30) wa kanisa la Pentekosti huko Nnewi, Nigeria amejiua kwa kujirusha kutoka kwenye jengo la ghorofa mbili na kufariki papo hapo kisa ni wivu wa kimapenzi. Ndugu wa mchungaji amesema Prosper alitumia pesa nyingi sana kwa mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano ikiwemo kumsomesha chuo kikuu kwa makubaliano ya kuja kuoana wawe rasmi mke na mume
Ila baada ya hapo mdada husika akamsaliti mchungaji huyo pia kukataa kuolewa nae hali ambayo ilimpa mshtuko wa huzuni kubwa na kujiua ikifikiriwa pia gharama kubwa alizozitumia kwa muda mrefu
Amejiua mwezi uliopita isipokuwa amezikwa Ijumaa hii kijijini kwao, lakini hata hivyo, ndugu ameeleza kwamba amezikwa kichakani kwasababu kufariki kwake kwa kujiua ni kinyume na mila za kijiji chao hivyo ni kama amekufuru.