Ni mauaji ya kinyama! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwalimu wa Shule ya Msingi Nyakatundu iliyopo Rufiji mkoani Pwani, Rafaela Msemwa kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Agosti 6, mwaka huu.
Pamoja na kutekeleza unyama huo, watu hao pia walimjeruhi mtoto wake mwenye umri wa miaka minne, aliyejulikana kwa jina la Bravian Mwamwenda na kumsababishia jeraha kubwa usoni na kwa sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mpaka sasa Bravian ameendelea kupokea matibabu kutoka kwa wataalamu bingwa na tayari wamemfanyia upasuaji wa jicho na wanasubiri kumfanyia vipimo vingine kuangalia iwapo jicho hilo litaweza kuona tena.
View attachment 2714034
Sent using
Jamii Forums mobile app