Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Endelea kuifungua mama 🙏🏿

JamiiForums934640752.jpeg
 
Kabisa kabisa...

Nikataka ku-hack account yake. Yaani ilibakia kubofya tu mara moja na ningeweza kusoma meseji zake za WhatsApp, meseji za kawaida na akaunti zake nyingine. Moyo ulikuwa unadunda. Kijasho jembamba...nitakutana na nini huko?

Ndipo kisauti fulani cha busara kikaninong'oneza: Kama hauko tayari kumuacha huyu mwanamke basi acha unachotaka kukifanya maana utaumia sana. Polepole nikaiweka simu chini. Moyo ulikuwa unapiga hatari.....nilikuwa nahema!

Nafurahi kwamba niliisikiliza sauti ile ya busara maana kusema kweli siwezi kumuacha huyu binti wa Kingoreme. Nimeshajaribu zaidi ya mara sita lakini naishia kuumia sana na kurudi kujisalimisha. Sijui kanifanyia nini huyu malkia jamani!

➡️➡️➡️ Usifanye jambo lo lote kama matokeo yake yatakuumiza na hutakuwa na la kufanya mbali na kumwachia Mungu. ZINGATIA sana ushauri huu utakusaidia

IMG_20230716_233529_409.jpg
 
Dear Mama E

Kama morani hodari akitavyo mkuki wake mbele ya kibanda cha rafiki yake ili kutangaza himaya na uwepo wake pale. Nami naukita mkuki huu mbele ya mlango wa moyo wako mwema ewe malkia wa Kingoreme.

Kwa mkuki huu nautangazia ulimwengu kuwa wewe ni wangu jana, leo, kesho na hata milele. Hebu mkuki huu na unachokiwakilisha vikaheshimiwe na si na wewe tu bali na kila mtu. Sisi ni himaya moja Mngoreme wangu!

Ubarikiwe daima!

v.u.n.j.a.m.b_a.v.u_20230624_113.jpg
 
Back
Top Bottom