dogo mmoja wa zama hizi,alikacha shule akakimbilia mji mwingine,baada ya muda akapata mwenza wakaoana wanavyojua.maisha yakaendelea,kule nyumbani alipotoka baba alibaki peke yake,kwani mkewe yaani mama yake dogo,alishafariki.katika kutibu upweke,baba akatafuta binti,akaoa,maisha yakaendelea.baada ya miaka kadhaa,dogo akakumbuka nyumbani.wakati huo,baba na na binti walishapata mtoto,dogo nae na mkewe pia walishajaliwa mtoto.safari ikaandaliwa kurudi nyumbani kijijini.walipowasili nyumbani,furaha ikaigubika nyumba ya kina dogo kwani ni kitambo toka alipoondoka.pamoja na furaha baba yake dogo alionekana kumtazama sana,mkwewe,kiasi alianza kumpa mawazo dogo,aliwaza au baba anamuona mkwewe mzee?maana kwa macho tu dogo alionekana mdogo kwa mkewe.wakati wote huo mama wa kambo wa dogo alikwenda kuchota maji,kilomita kadhaa toka nyumbani.hatimae akarejea.ila kurejea kwake kulileta hali isiyokua na majibu.alipotua ndoo tu na kwenda kuwaona wageni,aliangua kilio kisicho cha kawaida,mkewe dogo nae,akaonganisha,mwanzoni baba dogo na dogo,walidhani,wanawake wanachanga machozi,wakiwa hawaelewi ,ilibidi kila mmoja ambembeleze wake,ili watambulishane,wakati huo watoto wakiwa wamepishana umri kidogo sana,walikua wakicheza sakafuni ama vumbini,hapohapo sebuleni.kilio kilipoisha mke wa alianza kwa kumuomba dogo msamaha kwani,hakuwahi kumueleza kua ana mtoto.ila alipata mimba akiwa darasa la tano.na mwanae baada ya kupata kimo tu.alitoroshwa kijijini.na mtoto mwenyewe ndio huyo mke wa baba yake.ikabidi dogo,na baba yake,akili ziwaruke kwa muda hasa wakiwaza utambulisho wao unakuaje,yaani mke wa dogo ni mama mkwe wa baba dogo,hivyo dogo anakua baba mkwe wa baba yake,kisha mama yake dogo wa kambo ni mwanae wa kambo,na mama hivyohivyo mwanae wa kambo ni baba yake wa kambo kizaa zaa zaidi ni kwa watoto,kwani mtoto wa dogo,bibi yake wa kambo ni dada yake wa kuzaliwa,na babu yake ni shemeji yake.na mtoto wa baba dogo,dogo ni kaka yake baba mmoja,ila pia ni mume wa bibi yake hivyo ni babu yake.na bibi yake pia ni mke wa kaka yake hivyo ni shemeji yake,na watoto wakikua mdogo wake dogo mtoto wa kaka yake ni mwanae,lakini kazaliwa na bibi mzaa mama hivyo ni mjomba,na mtoto wa dogo,mdogo wake dogo ni baba yake,lakini kazaliwa na dada hivyo ni mpwa wake.yaani dogo, aligeuka mkwe,shemeji,mwisho akawa babu yake mwenyewe.hatari sana kuoaoa tu bila taarifa.
Sent using Jamii Forums mobile app
