UCHAWI UPO HADI KWENYE U MC DHA
"Ni kweli nilirogwa, ishu ilikuwa hivi, nimetoka nyumbani na gari yangu mwenyewe ile nafika ukumbini nakuta vyombo siyo vyangu na mazingira ya ukumbi siyo yangu, nilichokifanya niliwapigia vijana wangu simu kuwauliza wako wapi, waliponiambia wako sehemu fulani ilibidi niwashe gari tena kwenda kwenye ukumbi wangu, na hizo kumbi moja ilikuwa Mikocheni na ukumbi mwingine ulikuwa Sinza"
"Siku nyingine maiki iligoma kabisa kutoa sauti, nilipomgia MC mwenzangu mkongwe akaniambia bwana hapo umerogwa, mimi nimeacha hiyo kazi kwasababu kuna uchawi sana kwenye kazi ya u MC, hapo ndio nikajua kumbe nimelogwa, kuna mpiga picha mwingine aliniambia aliacha kazi ya kupiga picha kwenye sherehe kwasababu alikuwa anapiga picha vizuri, lakini akirudi nyumbani ili kuzisafisha kwenye kadi hazionekani, akaniambia kwenye hizi kazi kuna uchawi mkubwa sana"
"Juzi video yangu iliposambaa niliposema narogwa, kuna Mganga kutoka Kilimanjaro alikipigia simu akaniambia amesikitika sana na mimi kurogwa, akasema nimpe siku saba amzike MC anayeniroga ili watu waniheshimu lakini nikamwambia hapana, ngoja tumuachie Mungu, ila kiukweli kwenye hizi kazi kuna changamoto sana"- Dr. Cheni
ALIYE post
ni admin wangu

Djparty On Mix
View attachment 2641546
Sent using
Jamii Forums mobile app