Kampuni ya kutoa Mikopo kwa Njia ya Mtandao ya #WhitePathLTD, imepigwa faini ya Ksh. 495,614 sawa Tsh. Milioni 8.6 kwa madai ya kuingilia na kutumia taarifa binafsi za wateja kufuatilia wadeni wake.
Ofisi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ilisema ilipokea takriban malalamiko 150 dhidi ya kampuni hiyo ikidaiwa kuwapigia simu ndugu na jamaa wa wadeni wao wakiwataka kuwakumbusha kulipa madeni.
Wafanyakazi wa Kampuni hiyo pia walishutumiwa kwa kuwanyanyasa na kuwatukana walalamikaji na marafiki zao kupitia namba za simu zilizopo katika nyaraka zao za kujiunga katika huduma hiyo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.