Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

FB_IMG_1675367188529.jpg
 
Ngoja nikupe kisa cha kweli.

Mwaka 2010 nilibahatisha pisi kali hatari mitandaoni humu humu - picha kali hatari tena mno pisi inadai kuwa iko 27 yrs. Halafu tipwa tipwa imefungasha sijaona...kama nipendavyo!

Siku ya kuonana sasa. Kumbe ni mama mtu mzima sana 45yrs+ halafu kachoka choka hatari. Tulienda kwenye mkahawa mmoja tukala na kuongea vizuri namuuliza kulikoni mbona yanayopaswa kuwemo hayamo? Oooh zile picha nilikuwa natumia za binti yangu na blah blah kibao..mpaka tukaagana jioni nikampa na nauli ya kurudia huko Kibaha ndani ndani huko.

Ila tuliishia kuwa marafiki sana siyo na yeye tu bali hata mabinti zake wawili akiwemo yule mkali kabisa ambaye picha zake ndiyo nilikuwa natumiwa. Hata mama yao alipofariki nilikwenda kwenye msiba.

Mitandaoni humu unaweza kuwa catfished...na ni vyema kuwa mwangalifu. Tangu kisa kile kinitokee niko makini hatari!

RIP Mama Ashura
Hukulaga kweli akina ashura wewe
 
Back
Top Bottom