Habari zenu ndugu walimu wenzangu?
Hongereni sana kwa kazi nzuri ya usimamizi wa mitihani ya kuhitimu Elimu ya msingi( PSLE 2022.)
Ni imani yangu kwamba kazi hiyo imefanyika Kwa ufanisi mkubwa sana, narudia kusema kwamba hongereni sana kwa kazi nzuri.
Nimeamua kuandiaka ujumbe huu kwa lengo la kuongelea ukarimu kwa wasimazi( HOSPITALITY)
Asilimia 90 au zaidi ya wasimazi wa mitihani hii ya msingi kwa Sasa ni walimu wa Secondary na asilimia inayobaki ni wasimazi waliotoka shule za msingi.
Wenzetu walimu wa Secondary nadhani mmeona ukarimu wa walimu wa shule za msingi, mmekula, mmekunywa na kulala pazuri.
Namna mlivyoandaliwa na kuhudumiwa chakula pia inaridhisha sana.
Lakini pia walimu wenzenu wamewachangamkia sana.
Ila inapokuja kwenye mitihani yenu, walimu wa shule za msingi wanapokuja kwenu kusimamia kuna aina fulani ya dharau inakuwepo.
Kwanza chakula kinapikwa kibovu, kidogo, alafu chakula cha usiku ( dinner) hakuna kabisa badala yake walimu wanaenda mitaani kutafuta vyakula au wanalipishwa hela ili kununua chakula na kumlipa mpishi.
Nataka nitoe mfano kwakuwa walimu hata mwaka Jana walikutana na issue za dharau sana, mfano walimu kutopata hata maji ya kunywa



inauma.
Kuna walimu waligawana chai ya rangi nusu kikombe,
Walimu kusimamia mitihani huku wakimaliza wanaenda kuhangaikia mboga au chakula cha jioni.
Kwa kifupi ni kwamba haya ambayo wasimazi wa msingi wanafanyiwa hayapo Secondary.
Nataka niwaambie kwamba hatuwakarimu labda kwakuwa tunawaogopa hapana!
Ila ukarimu ni sehemu ya maisha yetu.
Ufike wakati walimu wa Secondary fikisheni taarifa kwa wakuu wenu wa shule ili mfanye kama mnavyofanyiwa huku.
Kwanza hela hizo za kulisha wasimazi sio zao ni pesa za serikali.
Kuna hoja moja kwamba shule za msingi mitihani inafanyika kwa siku chache na Secondary mitihani inafanyika kwa siku nyingi, ndio maana walimu wanaoenda kusimamia Secondary hawakarimiwi chakula usiku na mchana.
Hoja hii ni dhaifu sana,
Naweza kusema kwamba wasimazi wanaokuja S/M ni wengi sana kuliko wanaoenda Secondary.
Mfano hata shule ya Secondary yenye wasimazi watatu nao walikosa hata maji ya kunywa kwa siku Saba, lakini shule ya msingi yenye wasimazi Saba walikula kwa siku tatu asubuhi, mchana na jioni.
Nawatuma walimu wa Secondary walioenda kusimamia msingi fikisheni ujumbe huu kwa wakuu wenu wa shule.
Acheni dharau, ubinafsi na kujiona sana.
Onyesheni upendo.
Kwanza shule za Secondary zinaruzuku kubwa kuliko za msingi,
Alafu suala la mitihani si suala la ghafla kwanini msijipange mapema?
Hamuoni aibu walimu wenu wanavyokarimiwa alafu nyie mnawafanyia tofauti hivyo?
Tusifike mbali, naomba mitihani ya FORM TWO & FOUR 2022 haya mauzauza yasiwepo tena.