Shilingi noma:
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe, hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu ndogo, sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.
Baada ya simu kukatwa mke akamgeukia mumewe:
Mke:, ”eenheee!!! ulikuwa unasema umenichoka nikusanye nguo zangu halafu iweje?
Mume: (kwa upole sana, tena kama siyo yeye vile) “Baby wangu, mpenzi wangu, mama watoto wangu, honey wangu mtamu, Laaziz... nikuambie kitu? ...nilikuwa nasema tu, unikusanyie nguo zako zote chafu unipe nikusaidie kufua angalau kwa leo tu nijikumbushie... Si unajua mambo ya mahaba moto moto tena...”😊