Karaha ya kuzamia sherehe ya watu!
Pale unapozamia Dinner Party ya Jumuiya Fulani, kumbe Lengo lao ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiya…sasa unakaa mbele kabisa ili Muda wa
Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage tuu!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Makete, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai, nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisa….papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!…Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mwengineee?”
Kimyaaa…
Haya jamani kama hakuna Ofa ingine Papai linakwenda kwa Rweyemamu!……..
MC: Haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!” ( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”)
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!….ofa nyingineeee!”
Kimyaaa…
MC: Jamani, jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!…ofa nyinginee!
Kimyaaa….
MC: Jamani ofaaaa!
Kimyaaa….
Hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB ni zero balance… Sasa unageuza macho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo, kumbe anachezea tu simu... Unamcheki Rweyemamu Kwa kuibia, kumbe anatafuna tu kitu hata hana habari🙄
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa mafanikio makubwa...
MC: Mpatieni Kabasele Jogoo lake!
Hapa sasa unapokea jogoo lako la MILIONI kwa Tabasamu la HUZUNI kuuubwa….kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba
John Cena😳
Wakati unaongozwa kwenda kwa cashier kulipa milioni, unahisi kama mazaga zaga uliyokula yanataka kutokea masikioni!!!