Ndoto za wanafunzi
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanaopenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua mfano mzuri kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Pia nimiliki Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa.
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeheshimika. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza.
Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah😊