Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Tamaa​

Muokota makopo katika uokotaji wake akaona chupa ambayo ndani kuna kitu, alipoifungua likatoka jitu la ajabu.

Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vitu viwili sasa hivi..

Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari.

Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka pale..

Akaambiwa sema ombi la pili ambalo ni la mwisho, akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada woote!

Hapo hapo akageuzwa akawa
chipsi yai😊
 
Apo ngoja kwanza ncheke😂😂😂
 
Mchungaji​

Mchungaji kamfuata pedeshee moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;

MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga Kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na
utabarikiwa zaidi..

PEDESHEE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza unga.

MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo pekee, we toa tu😊
 
Ashura mbona hivyo?
1659762243104.jpg
 
Tamaa​

Muokota makopo katika uokotaji wake akaona chupa ambayo ndani kuna kitu, alipoifungua likatoka jitu la ajabu.

Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vitu viwili sasa hivi..

Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari.

Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka pale..

Akaambiwa sema ombi la pili ambalo ni la mwisho, akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada woote!

Hapo hapo akageuzwa akawa
chipsi yai
 
Ndoto za wanafunzi​

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanaopenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua mfano mzuri kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Pia nimiliki Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa.
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeheshimika. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza.
Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah😊
 
Degree​

Jamaa mmoja kahitimu chuo ana degree moja kaenda kuomba kazi Kwa kiwanda cha Mhindi..

Jamaa: nina degree moja natafuta kazi, je kuna nafasi?
Mhindi: ndiyo, kuna kazi ya kupakia mzigo kwenye Lori la kusambaza bidhaa zetu mikoani huko.
Jamaa: hapana, siyo hiyo, natafuta kazi ya uhasibu maana nina B.Com (Accounts).
Mhindi: hapana kazi... mtu iko degree 1 pekee nachagua kazi? Thermometer iko degree 100, Lakini inafanya kazi kwenye kwapa🙄
 
Padri Asepa wakati wa kuungamisha​

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sanaaa.”

Padri, “Endelea…”
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaa….
“Padri yesu atanisamehe?”
kimya….

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umenikimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu…….🙄”
 
Mimba​

Jamaa: Mambo honey, upo ok?
Mrembo: Sipo ok my dear
Jamaa: Una tatizo gani baby?
Mrembo: Nimetoka hospitali kupima, nna mimba.
Jamaa: Weeeh, thubutu... usiniletee balaa hiyo mimba imeingiaje wakati huwa tunatumia kinga?
Mrembo Kwani nani kakwambia mimba ni yako, hebu tuliza mshono huo🙄
 
nimekumbuka story ya jobless mmoja, ilikuwa asubuh anaamka anaswaki vizuri, mafuta mengi anatoka zake vizuri tu kama anaenda sehemu kwenye kazi kumbe anaenda kuzurura barabarani au anaenda uwanjani anakaa huko saa tatu hivi au saa nne washua wakiwa washasepa nayeye ndio anarudi home kumalizia usingizi. Mjini hapa anakwambia usikae kizembe
 
Tamaa​

Muokota makopo katika uokotaji wake akaona chupa ambayo ndani kuna kitu, alipoifungua likatoka jitu la ajabu.

Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vitu viwili sasa hivi..

Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari.

Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka pale..

Akaambiwa sema ombi la pili ambalo ni la mwisho, akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada woote!

Hapo hapo akageuzwa akawa
chipsi yai
halafu jini likasepa halina muda wa kupoteza!
 
Back
Top Bottom