Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Sisi watanzania ni watu pekee tunaotoa indozement kwa watu waliofeli badala ya waliofanikiwa,, walioshindwa badala ya waliofaulu, wajinga badala ya werevu. Tulisha tengenrza masuper star wa hovyo hukonyuma bila sababu za msingi,, tulishatengeneza super star mlavi,,(Piere liquid)tukawatengeneza kina miatisa itapendeza(Dr Shika) na wengine wengi tu.

Leo tunarudi mulemule kumpa umaarufu mbwatukaji aliezunguka mitaani na magari yakiofungwa vipaza sauti akiwaomba watu kwamba liandaliwe kaburi mana atamuua opponent wake ulingoni badala yake akadundwa yeye kwa K.O nusura auwawe.

Cha kusikitisha leo hii aliedundwa na kutaka kuuwawa ulingoni ndio kawa maarufu kuliko aliemdunda. Ndio anaezungumziwa sana na. Mitandao ya kijamii kuliko mshindi wa pambano lile. Ndio anaepewa airtime kubwa na vyombo vya habari ikiwemo magazeti na television kubwa tu hapa nchini zinamuialika aliepigwa studio na kufanya nae mahoiano live kuliko shujaa aliempiga huyu mbwatukaji.

Namna hii tunaharibu maana nzima ya ushindi na ubigwa na tunaweza kutengeneza kizazi kitakachoamini ukitaka kuwa star kwa haraka basi uwe bondia na uwe mbwatukaji na ukiingia ulingoni udundwe.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana.

C&P Shangazi Fatu
 
FB_IMG_16596126919470991.jpg
 
Back
Top Bottom