Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Mjini shule..​

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea.

Baada ya wiki nampigia simu hapokei, nimempigia zaidi ya mara 10 kimyaa!

Nikaona isiwe shida nikamwandikia message kwa WhatsApp:

"Hello Mum, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba N). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama hana akili nzuri.."

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu mfululizo kama mara 20, mie kimyaa..

Akatuma message:
"Hao wanawake unawajuwa, …mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli…!"

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa…!

Akanipigia tena simu mara 5, mie kimyaaa…!

Akaniandikia message nyingine:
"Best, nakupigia jamani pokea simu basi, nina pesa zako hapa nataka nikupe… Naomba basi tukutane mjini unisimulie vizuri…!"

Mimi:
Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke kabisa mahala walipo…!

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza na inasoma pesa zangu zote ninazo mdai…!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa…. Kama sio mie vile😊
 

Mume mlevi:​

MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo refu la Maji nife kabisa.
MKE. Kufa tu maana huna faida yoyote duniani!
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga haraka, kafungua mlango katoka nje na kwenda kuchungulia shimo. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE
: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Sawa, piga kelele tu na wakija uwaambie ulikuwa wapi usiku wote huu na khanga moja😊
 
Screenshot_20220705-100803.jpg
 
Back
Top Bottom