Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

Mmmmh
FB_IMG_16501185426703202.jpg
 
APEWA SIKU 15 ARUDI URAIANI, AMPE MKE WAKE MIMBA KISHA ARUDI JELA

Jamaa anayetumikia kifungo cha maisha jela mahakama yampa ruhusa siku 15 kurudi uraiani kumpa mimba mke wake kisha arudi jela

Mwanaume husika kwa jina la Nandlal(34) , mke wake kwa jina la Rekha ameenda kuililia mahakama ya Jodhpur/Rajasthan nchini India akitaka apewe mimba na mume wake anayetumikia kifungo cha maisha jela

Mahakama iliamua kupitia vifungu kadhaa vya sheria na imani mbalimbali za kidini ikiwemo Uhindu, Ukiristo, Uislamu, Judaism na kuona mojawapo ya mambo muhimu katika maisha ni pamoja na mtu kuendeleza vizazi/koo pale anapoamua iwe hivyo ndio Rekha akasikilizwa ombi lake

japokuwa mume huyo amefungwa maisha kwa makosa yake lakini kwa upande mwingine mahakama imeona hali hiyo imemuathiri mke wake kihisia na haki yake ya kupata tendo la ndoa licha ya kuwa yeye mke hana makosa yoyote ndio maana amesikilizwa

Pia imeelezwa, kipindi cha nyuma mahakama ilimpa mwanaume huyo ruhusa ya kwenda uraiani kwa siku kadhaa halafu muda ulipoisha akarudi mwenyewe jela kuendelea kutumikia kifungo chake cha maisha hivyo alionesha nidhamu na utii wa sheria ndio maana wamempa tena siku 15 arudi uraiani kumpa ujauzito mke wake afurahie maisha yake na ya ndoa halafu mume arudi zake gerezani

Follow hii page kwa Habari zaidi
#JAYSADIAN___UPDATES
 
Back
Top Bottom