Nilijaribu kutumia kila njia ili nimtoe ndugu yangu kipenzi Ismail Ally Abubakar kwa huyu mama anayejiita mungu chini,lakini kila mbinu niliyoitumia hakika iligonga mwamba,ilifikia hatua mbayo Ismail hakutaka kabisa tuongelee swala la imani yake juu ya huyo mungu wake ambaye yeye anadai hakika ni mungu wa kweli kwake.
Ilibidi nichukue muda wa kukaa na ndugu yangu ili nimuulize ilikuwaje akaaminishwa imani potofu kama ile,imani ambayo ni wazi kabisa inapingana na Kristo,lakini ndugu yangu alinijibu kuwa;huyu Zumaridi ni mtu ambaye anakushika mkono na kutazama kiganja chako,kisha anakwambia matatizo yote yanayokuhusu wewe.
Nadhani hii si mara ya kwanza kwa mwanamke huyu anayejiita Zumaridi mungu chini ya jua kukamatwa na polisi,nakumbuka enzi za Magufuli akiwa hai,kanisa la mama huyu liliwahi kufungiwa na serikali,hivyo mimi nikanyanyua simu na kumpigia ndugu yangu Ismail na kumuuliza kulikoni mbona mungu wenu kanisa lake limefungiwa?
Ismail alinijibu kuwa;hayo ni mapito ambayo mungu wao ni lazima ayapitie,maana hata Kristo alipingwa sana na alikamatwa akapigwa na kutemewa mate,lakini kuteswa kule kwa Yesu hakukumaanisha kuwa yeye sio nabii wa Mungu hapana,bali ile ilikuwa njia ambayo ilimpasa Yesu kupitia ili kutimuza unabii wake.
Nikamtania Ismail kwa kumwambia,sasa kama huyo kweli ni mungu wenu,je siku akiugua ama akiingia period huwa mnamwabudu vipi

Au mungu mke huyu akiugua mumewe huja kuwa mungu badala ya mkewe?
Ismail akanijibu kuwa;mungu wao Zumaridi huwaambia kuwa,sababu ya Yesu Kristo kutokuwa na mke duniani ni kwa sababu wanawake wa zamani hawakujua kuoga,kuvaa na kujipamba,hivyo Zumaridi anadai kuwa hata Yesu akija leo hii lazima apeleke posa kwao na Zumaridi
Kiukweli nilifanya kila njia kumuokoa ndugu yangu,ila niligundua kuwa Zumarudi alikwisha waathiri kisaikorojia,hivyo kuwatoa vitu ambavyo kawapandikiza ndani yao ni ngumu sana labda kwa uwezo wa Mungu tu,ikafikia hatua mimi na Ismail ambaye ni binamu yangu tukawa hatupigiani hata simu kabisa.
View attachment 2136343