Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

IMG-20211118-WA0287.jpg
IMG-20211118-WA0252.jpg
 
Huyo jamaa ndiye nani?
Mbona hafanani kabisa na mwanzilishi na mmiliki wa SANI Said Bawji!!

Sent from my SM-J810F using JamiiForums mobile app
RIP Nicco Ye Mbajo

Tasnia ya Bongokomiki imepata pigo baada ya mmoja kati ya wachoraji wakongwe nchini Mzee Nicco Ye Mbajo kufariki dunia. Mzee Mbajo amefariki dunia usiku Jumamosi kuamkia Jumapili ya juzi jijini Dar es salaam.

Jina la Nicco Ye Mbajo linaweza kuwa geni kwa baadhi ya wapenzi wa Fasihi kutokana na kuwa kimya kwa kipindi kirefu kidogo lakini kazi za ubunifu wake hazijawahi kuacha kujulikana na mpenzi yeyote wa majarida ya kiswahili nchini.

Sidhani leo kama yupo Mtanzania yeyote mpenzi wa kusoma majarida ya Kiswahili nchini asiyelijua Jarida la SANI ambalo nathubutu kusema ndiye Baba wa Majarida yote ya burudani na vikaragosi nchini tangu mwanzoni mwa miaka ya 80.

Jina la SANI lilikuwa ubunifu wa muunganiko wa kifupi cha majina mawili ya mwanzo ya waasisi wa Jarida hilo ambao ni marehemu Saidi Bawji na Nicco Ye Mbajo, yaani SA (Saidi) na NI (Nicco). Marehemu Nicco ye Mbajo ndiye alikuwa mchoraji wa kwanza kabisa wa SANI.
Amezikwa Jana tarehe 17/11/2021 makaburi ya kinyerezi, bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Nimemkumbuka ingawa kwenye ubunifu wa picha hakuwa peke yake.
Pamoja naye kulikuwa na mkongwe aliyejulikana kwa jina la Philip Nduguru RIP.
Ndugu Mbajo baadaye alianzisha jarida lake ambalo hata hivyo halikutamba.
Baadaye alipata kazi kwenye Kanisa moja hapa mjini akiwa kama msemaji wa Askofu.
Amepotea muda mrefu kwenye tasnia ya majarida
 
Back
Top Bottom