Vituko mitandaoni. Tupia chako

Hebu tukumbushe huyu jamaa alikuwa nani na ana maajabu gani?
Huyu jamaa amesimuliwa kwenye masimulizi ya mtunzi wa kale Sir Henry Rider Haggard.(Mambo ya ajabu yaliyowapata Allan Quatermain na wenzake).
Anaitwa Umslopogas.
Huyu mwamba ameelezewa kama mfalme jasiri na mwenye nguvu wa Wazulu, aliyepoteza himaya yake kwa sababu za kimapenzi.
Kwa sababu hiyo akatorokea Afrika mashariki kukwepa kifo.
Akaja kukutana na msafara wa rafiki yake wa zamani, mwingereza mwindaji aitwaye Allan Quatermain.
Kwakuwa aliogopa kurudi kwao, aliungana na msafara huo kama kiongozi wa wapagazi (Wabeba mizigo).
Kwenye msafara huo amefanya mambo mengi ya kijasiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…