Mwaka 2002, maisha ya mzoa taka kutoka Uingereza, Michael Carroll, yalibadilika ghafla baada ya kushinda bahati nasibu ya UK National Lottery yenye thamani ya pauni milioni 9.7, sawa na takribani shilingi bilioni 31 za Tanzania.
Baada ya ushindi huo, aliondoka kazini na kuanza maisha ya kifahari, akimiliki magari ya kifahari, kuishi kwenye majumba makubwa na kuandaa sherehe zisizoisha.
Hata hivyo, maisha ya anasa hayakudumu. Ndani ya kipindi cha miaka minane tu, fedha zote zilikwisha kutokana na matumizi yasiyo na mpango, uwekezaji ulioshindikana, na matatizo kadhaa na sheria.
Baada ya utajiri wake kuisha, Carroll alijikuta hana tena chochote, na akaamua kurudi kwenye kazi yake ya awali a kuzoa taka.
Leo hii, anaïshi maisha ya kawaida tena, akionyesha kwamba utajiri peke yake hauwezi kununua furaha bali ni busara katika matumizi ndiyo inayohakikisha ustawi wa kweli.