Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

1712767159368.png


(01) Mshahara umechelewa mwezi huu.

(02) Biashara yangu imeyumba kipindi hiki cha Uviko-19.

(03) Mwezi huu nimelipia bili ya umeme na maji na ada za watoto, hivyo sina hela yoyote kwa sasa.

(04) Benki itakuwa kuna fedha wamenikata, salio limepungua sana mpaka nifuatilie kwanza.

(05) Nina kiasi kidogo sana hiki hapa, kinachobaki naomba nilipie nikipata.

(06) Sherehe za krimasi na mwaka mpya zimefilisi, ninaamini mwezi ujao nalipa fedha yote inayobaki.

(07) Nilipanda pikipiki fedha zote zimedondoka ndio maana macho yangu yamekuwa mekundu hivi, nina mawazo mengi sana hapa.

(08) Nimetoka kuuguza bibi, sina fedha yoyote hapa.

(09) Nililipa kodi ya mwezi huu, itakuwa umejisahau.

(10) Nimepoteza waleti yangu, ilikuwa na kila kitu. Fedha ya kodi niliiweka kwenye waleti ili nije nikulipe leo.

Pumzika Kidogo Kabla Ya Kuendelea…

(11) Bado sijapata kazi, naomba nivumilie kidogo.

(12) Nimekosea kutuma fedha wakati nakutumia kwenye namba yao ya mtandao wa Vodacom.

(13) Nimepewa talaka, nahitaji muda wa kutuliza akili yangu.

(14) Mwenza wangu amenitelekeza, hivyo sina fedha hata kidogo ya kulipia chumba.

(15) Nina fedha kwa ajili ya kulipia kodi ya mwezi huu tu. Kodi ya miezi mingine nitamalizia.

(16) Bado sijapata kazi, naendelea kutafuta kazi.

(17) Mama amesema atanitumia fedha kwa ajili ya kodi ya awamu hii.

(18) Ndio nafika leo nilikuwa likizo na familia yangu. Nitakulipa nikipata fedha

(19) Dirisha la chumbani kwangu walivunja, wameiba fedha yote ambayo nilitunza kwa ajili kodi ya nyumba.

(20) Mkewangu ana mimba ninatumia kiasi kikubwa cha fedha kumnunulia chakula atakacho.

Pumzika Kidogo Kabla Ya Kuendelea…

(21) Nilienda fiesta ya msanii wa kimataifa, gharama zilikuwa kubwa kuliko nilivyotarajia. Nitakulipa mara baada ya kupata fedha nyingine.

(22) Nguruwe wangu amekula waleti/pochi yangu na fedha zilikuwa kwenye hiyo pochi.

(23) Bosi wangu amesema atachelewa kunilipa mshahara wa mwezi huu.

(24) Nilisahau. Nilijua nimelipa kodi ya mwezi huu. Naomba nitafute kwanza.

(25) Nimefungua kampuni ya biashara zangu. Hivyo sina fedha yoyote hapa.

(26) Nimetoka kujumua bidhaa za biashara yangu, sijabakiwa na kiasi chochote kwa ajili ya kodi.

(27) Mashine ya ATM ilimeza kadi yangu ya benki toka juzi. Nasubiria wanitolee ndipo nitoe fedha.

(28) Mume wangu amesafiri kidogo, yeye ndiye huwa anatunza fedha kwa ajili ya kodi ya nyumba.

(29) Sitalipia kodi ya mwezi huu, ninahamia nyumba ya kwa Mzee Mwakyembe.

(30) Tumetoka kufunga ndoa na mkewangu. Fedha yote ilitumika kwa ajili ya harusi.

Pumzika Kidogo Kabla Ya Kuendelea…

(31) Nilikokuwa nimepanga toka mwanzo nilizoea kuchelewesha wiki moja hadi tatu.

(32) Mpenzi wangu ametoroka na amenitapeli fedha zangu zote na nguo zangu zote.

(33) Hivi nadaiwa shilingi ngapi hadi mwezi maana sina chochote hapa?.

(34) Nilikutumia ujumbe kwa njia ya simu kuwa mwezi huu nitachelewa kidogo kulipa kodi. Je hukupata ujumbe wangu?.

(35) Jana pikipiki yangu ilipigwa faini kwa makosa ya barabarani, hivyo sina fedha yoyote muda huu.

(36) Mtandao wa benki kwa njia ya simu unasumbua, benki ipo mbali huko mjini.

(37) Sikubali kulipa kodi ya mwezi huu, mpaka upunguze kodi kama wengine wanavyofanya.

(38) Nimelipia kodi ya mwezi uliopita hata mwezi haujaisha unataka nikulipe kodi nyingine niitoe wapi sasa?.

(39) Mimi ni mwanafunzi, nyumba niliyekuwa nategemea anitumie fedha hajatuma mpaka leo hii.

(40) Mkewangu amejitungua watoto mapacha wawili, hivyo nimetumia fedha nyingi kwa watoto na mkewangu

Pumzika Kidogo Kabla Ya Kuendelea…

(41) Nimeachwa na mumewangu juzi tu, hapa kichwa kimevurugika kabisa. Naomba nitafakari vizuri.

(42) Gari langu liliharibika, fedha yote nimetumia kurekebisha gari yangu.

(43) Nililala klabu wikiendi hii, niliingia majaribu ya kutumia fedha yote niliyokuwa nayo.

(44) Nimetafuta mteja wa kununua Sabufa (Subwoofer) yangu sijapata hadi leo tangu mwezi uliopita.

(45) Ninataka niende kutafuta maisha Dar Es Salaam, hivyo ukipata mpangaji mwingine mlete kwenye chumba hiki.

(46) Uzalishaji wa bidhaa kiwandani kwetu umesimama kwa sababu ya jana la Uviko-19, mishahara hatulipwi tena.

(47) Watoto wangu watatu wameanza kidato cha tano mwezi huu. Hapa nilipo sina fedha yoyote.

(48) Mkewangu ametumia fedha ya kodi niliyotunza, alikuwa hajui kuwa ni akiba ya kodi ya nyumba.

(49) Silipi kodi tena mpaka ufanye ukarabati wa paa inayovuja huku chumba cha kulala.

(50) Sitalipa kodi nyingine mpaka uje na mkataba mpya kama tulivyosaini mwanzoni.
 
Back
Top Bottom