TAIFA LINALOTEGEMEA LISHE YA KUPEWA NI TAIFA MFU.
Disemba 2023 serikali ilifuta taasisi ya chakula na lishe Tanzania (TFNC) iliyokuwa chini ya wizara ya afya halafu mnakwenda kuomba kusaidiwa lishe na mabeberu?
Miaka 61 baada ya uhuru lishe yetu na watoto wetu ni changamoto? Naibu Waziri wa Fedha anakenua meno Tanzania kusaidiwa lishe. Hivi, hii CCM mnaipendea nini watanzania?
Wizara ya Kilimo ya Marekani, imetoa msaada wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani kwa raia wa Tanzania.
Tunaagiza mafuta ya kula kutoka Malaysia, watu ambao walikuja Tanzania kuchukua mbegu za Michikichi Kigoma eneo la Bonde la Mto Luiche na kwenda kuzalisha nchini kwao,
Malaysia wanauza semi-refined, refined na crude-oil nje ya nchi ya nchi yao kuliko nchi nyingine yoyote ukanda wake (insular region of Southeast Asia). Walipata uhuru 1957
Kigoma wakiwezeshwa wanaweza kuzalisha Tani 200,000 za Crude palm oil (CPO) kwa mwaka. CPO ni mafuta ya mawese ambayo hayajasafishwa, yanayoka kwenye chikichi.
Tanzania kwa mwaka tunatumia $340M sawa na TZS 789.6bn, zaidi ya bajeti ya maji na umwagiliaji ambayo ni TZS 727bn. Unajiuliza maswali mengi na huwezi kupata majibu.
Thamani ya fedha iliyotumika kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ni sawa na fedha ambazo wizara ya maji na umwagiliaji ilitengewa kwa mwaka fedha wa 2018/2019.
Lakini pamoja na kuwa Kigoma kuna uoto wenye kukidhi kilimo cha chikichi, bado ni kati ya mikoa maskini zaidi. Pesa za kupeleka Malaysia kwanini tusiwekeze Kigoma?
Russia wanawekeza si tu kwenye chakula na lishe kwa watoto bali wanawekeza hadi kwenye “chromosome”… ujauzito wa raia Russia ni mali ya nchi siyo jambo binafsi.
Russia wanafuatilia na wakigundua kuna kasoro yoyote kwenye malezi ya mtoto, hawaulizi mara mbili. Mzazi utaaanza moja kwa kufuata mwongozo wa serikali.
Rais wa Russia (1924-1953), Joseph Vissarionovich Stalin alitaka raia Russia wote wawe na muonekano na akili zinazoendana … ni nadra kukutana na DWARFISM Russia
Lishe duni nchi za Afrika ni mtaji kwa watawala. Ukosefu wa lishe bora unazaa udumavu wa akili. Udumavu wa akili unazaa taifa la watu wenye changamoto ya kufikiri
Ukiwa na watu wenye changamoto ya kufikiri ni mtaji. Fikiria ambavyo wananchi wanafikiri mwenezi wa CCM ni tofauti na watendaji katika serikali ya CCM. Wanampa kero.
Watu tuliowahi kudhani ni wasomi na wao kutokana na tatizo la lishe duni wanashinda wakitueleza ‘sasa CCM imepata mwenezi’ na wanamuona ndiye mkombozi halisi wa CCM.
Tembelea takwimu za nutrition status per regions. Linganisha na takwimu za ufaulu utagundua mikoa yenye NJAA kubwa inakua ya mwisho katika ufaulu. Fanya ulinganisho.
Tunaweza kuwa na nchi yenye watu milioni 62 lakini wenye uwezo wa kufikiri na kufanya kazi wakawa wachache, kutokana na udumavu na ukosefu wa lishe bora udogoni.
Watoto wenu wanakula vyakula visivyofaa (junk foods) kutoka supermarket. Hampiki. Uvivu. Mtoto ananenepa mwili, ubongo unasinyaa. Mwili mkubwa, akili ndogo.
Vijana wa vyuo vikuu wanawaza kuwa machawa. Hawana kitu kichwani. Wanashinda korido za Lumumba na kufanya press za kusema Rais apite bila kupingwa.
Hakuna fikra tunduizi vyuo vikuu. Hakuna midahalo mizito katika kumbi za vyuo vikuu. Hakuna mapinduzi ya fikra. Hata mikopo hawajui kudai. Wametulia kama broilers.
Breed broiler is any chicken (Gallus gallus domesticus) that is bred & raised specifically for meat production. Ndivyo wasomi wa vyuo vikuu sasa wanaandaliwa. KULIWA TU.
Tukiwekeza katika lishe bora tunakuwa na watu wengi ambao ni NGUVU KAZI na uchumi unakua. Vinginevyo tutakua tunazaaa “wapiga kura” na kutengeneza “machawa”
Suala la lishe ni usalama na ustawi wa Taifa lolote timamu. Suala la lishe ndiyo linaamua Taifa litakua na wananchi waliodumaaa mwili na akili mazezeta au werevu. Siyo mchezo.
Awamu ya kwanza tumetoka kutafuta uhuru, serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliweza kufanya uwekezaji mkubwa katika suala la lishe kwa watu wake.
Serikali ya Mwl, Julius K. Nyerere, kulikua na vyakula. Watoto wanakula shuleni. @IAMartin