Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

🤣🤣🤣🤣

FB_IMG_1709806098098.jpg
 
Mudi alikuwa na ndoo iliyojaa samaki wazima amepumzika pembeni ya mto Ruaha, mara mlinzi wa wanyamapori alimfata alipomuona amekaa pembeni ya mto.

Mlinzi wa wanyamapori alimwuliza Mudi, "Naweza kuona leseni yako ya uvuvi tafadhali?"

"Hapana" Mudi alijibu. "Sihitaji hata kuwa na leseni wala kibali, hawa hapa ni samaki wangu wa kufugwa."

"Samaki wa kufugwa?" Aliuliza Mlinzi.

"Ndiyo, mara moja kwa wiki na waleta samaki hawa hapa mtoni kisha nawaingiza mtoni waogelee kwa muda.

Muda ukifika wa kuondoka ninapopiga filimbi, wanaogelea kurudi kwenye wavu wangu na mimi nawachota na kurudi nao nyumbani."

"Acha usanii kijana, uko chini ya ulinzi kuanzia sasa." Alisema Mlinzi.

Mudi akasema, "Ni ukweli, nitakuonyesha ninafanya hivi kila wakati nikija hapa."

"Thibitisha" alifoka Mlinzi huyo wa wananyama pori.

Mudi aliwaweka samaki ndani ya mto na kusimama na kusubiri.

Baada ya dakika chache, Mlinzi wa wanyamapori akasema, "Sawa"

"Sasa nini?" Alisema Mudi.

Mlinzi wa wanyamapori akauliza, "Utawaita muda gani tena?"

"Niwaite wakina nani?" Mudi anauliza.

"SAMAKI" alijibu Mlinzi wa wanyamapori.

"Samaki gani?" aliuliza Mudi.

Mwisho
 
Back
Top Bottom