Vituko mitandaoni. Tupia chako

Vituko mitandaoni. Tupia chako

93460364005.jpg
 
Inaitwa MV Liemba meli iliyotengenezwa nchini Ujerumani mwaka 1913 kwa lengo la kutumika kama meli ya kivita kwenye Ziwa Tanganyika. Ilipokamilika iliwekwa kwenye makasha 5000 yaliyosafirishwa kwa meli tatu hadi Dar es Salaam. Kutoka Dar es Salaam ilisafirishwa kwa treni hadi Urambo ambapo ilibebwa na maelfu ya wapagazi hadi Kigoma ambapo iliunganishwa upya na kupewa jina la SMS Graf von Geotzen. Hili ni jina la aliyekuwa mmoja wa magavana wa Kijerumani Afrika Mashariki.
Katika kipindi chote cha Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Goetzen na meli nyingine za Kijerumani kwenye Ziwa Tanganyika kama vile Kingani na Hedwig von Wismann ziliwachachafya Wabelgiji na washirika wao Waingereza kwenye Ziwa Tanganyika na Wajerumani hawakuwa na mpinzani ziwani.
Vita vilipokolea na Wajerumani walipoamua kuuachia mji wa Kigoma, nahodha wa meli aliamua kuizamisha katika Ghuba ya Katabe mnamo tarehe 26 Julai 1916. Mnamo tarehe 16 Mei 1927 kwa amri ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo Sir Stanley Baldwin, meli hii iliibuliwa, ikatengenezwa na kupewa jina Liemba. Liemba bado ipo kazini miaka zaidi ya mia moja toka kuzaliwa kwake.



Credit Facebook
mvliemba.jpg
 
Back
Top Bottom