VITUKO: Mambo 20 yanayoonyesha una ukichaa wa mapenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
1. Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.

2. Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.

3. Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.

4. Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.

5. Kusema wanawake wote sawa.

6. Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.

7. Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.

8. Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!

9. Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?

10. Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!

11. Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!

12. Kumhonga mwanaume ili akuoe!

13. Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!

14. Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!

15. Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!

16. Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.

17. Kumsomesha mtu ili uje umuoe!

18. Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!

19. Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako!

20. Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..

Nimeipaste kama ilivyo kama imekugusa Nivumilie.
 
Kwa minajili hii ni kwamba asilimia zaidi ya 80 ya vijana wa kike na wa kiume ambao hawajaoa ama kuolewa wanahitaji msaada wa tiba. Vipi, hiki kichaa kinamlazimu mgonjwa apelekwe mirembe ama? Maana majengo hayatatosha kuwapokea wote.

Kazi ipo
 
Chaputa ndo suluhisho kwa wale mapenzi yanawaowatesa
79369562_1047005858977967_1496973819812773888_n.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa mujibu wa post yako kila mtu anakichaaa cha mapenz hadi wewe mleta mada japo huwezi weka wazi una kichaa namba ngapi
 
1. Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.

2. Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.

3. Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.

4. Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.

5. Kusema wanawake wote sawa.

6. Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.

7. Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.

8. Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!

9. Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?

10. Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!

11. Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!

12. Kumhonga mwanaume ili akuoe!

13. Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!

14. Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!

15. Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!

16. Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.

17. Kumsomesha mtu ili uje umuoe!

18. Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!

19. Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako!

20. Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..

Nimeipaste kama ilivyo kama imekugusa Nivumilie.
#8&13

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom