Vitu vya kuzingatiwa unapouza nyumba

JituParaTupu

Member
Nov 20, 2008
92
9
Habari wakuu,

Naomba kujulishwa vitu vya kuzingatia unapopanga bei ya kuuza nyumba ya kuishi.

Natanguliza shukrani.
 
Location,(karibu na barabara), maji na huduma nyingine..surrounding enviroment,je ni uswazi au uzunguni au shamba.
 
inafikika kwa gari, ina hati? Aina ya mjengo na eneo lillopo. Je ina bustani? Parking inaingiza magari mangapi?
 
3-roomed, ina hati, imepakana na barabara, ni uzunguni, parking ya kutosha fuso (ndogo) nane+ya gari ndogo ambayo ni ndani. eneo la bustani kubwa, mjengo ni for residential purpose, maji umeme tayari upo, ni fenced kwa wire,
 
Pamoja na yote hayo hayo jee haina tatizo la mirathi kama ni ya kurithi? jee haina mgogoro wowote na Banki? vitu vyote hivyo vizingatiwe kabla kupanga bei, katika siku za karibuni kuna nyumba iliuzwa mtaani hapo? iliuzwa bei gani? Nyumba iliyouzwa na hiyo yako zina utofauti upi?
 
jamani eti ni kweli ukiuza nyumba 10% ya mauzo inatakiwa irudishwe kwa serikali ya mitaaa au mama yangu anataka kupigwa changa la macho?
 
jamani eti ni kweli ukiuza nyumba 10% ya mauzo inatakiwa irudishwe kwa serikali ya mitaaa au mama yangu anataka kupigwa changa la macho?

mkuu

TRA ... kama kiwanja kina Title Deed ukifanya transfer lazima ulipe Capital gain Tax .... 10%
 
Wakuu,

Nyumba siyo ya kurithi na wala haihusiki na mgogoro wowotena benki. Mwenye nyumba anataka ahame, akaanze maisha mapya ya vijijini. Bahati mbaya sana hapo mtaani kwake hakuna nyumba iliyouzwa karibuni.
 
Back
Top Bottom