Vitu vya kuepuka kufanya ukiwa unaendesha gari ya Automatic

Yan gari ni lako umenunua kwa pesa zako alafu bado waja wanakuchangaya nalo mara usifanye ivi mara vile...
 
Kwani kuna mtu kasema usiweke full tank????
Bro.. Kuna watu ni wabishi kwa asili yao. hivyo usitumie nguvu nyingi kumu elimisha MTU kama huyo utamaliza ugali wa bure.
Ila kiasili ni kama una baisikeli umepakia gunia la 100kg kila unapo anza safari itakulazimu utumie nguvu za ziada mpaka upate mwendo ambao utaku sapoti.. Na gari IPO hivyo hivyo ikiwa full tank kwa mizunguko ya mjini tu. Inaongeza ulaji wa mafuta
 
42774277,
Nadhani watengenezaji wa magari huzingatia hili. Kama gari let say inatakiwa isizidiahe 1tone,wanahesabu mpaka full loaded tank. Zamani kulikuwa na kaswali "MELI INABEBA NG'OMBE 100, KATIKATI YA SAFARI HAO NG'OMBE WAKAJISAIDIA (HAJA KUBWA) JE! MELI ITAZAMA AMA ITAENDELEA KUELEA? Jibu likaja kuwa hicho kinyesi hakiongezi uzito wa meli
 
Hapo ukwaju kanishanga ipo 180kmh hiyo itakuwa gear gani? L , 2 au 3? Au Reverse? Sijamwelewa anaposema itabidi urudishe kwenye D

Sasa fundi mpaka gari imefika speed 180km/hr manake si ipo D automatically?au unadhan ipo gear gan kwenye auto unayoisemea?
 
Nina maswali mawili:
1.Neutral gear inatakiwa kutumika wakati gani?
2.Madhara ya kuacha gari ikatembea na Petroli chini ya nusu tank au ikiwa tayari taa ya mafuta imewaka, tukiacha hilo ulilosema kuwa inasababisha engine kutokupoa vizuri? Ninauliza hivyo kwakuwa nimeshashuhudia Taxi au Daladala nyingi zikifanya hivyo vitu na sikuona madhara kwa hayo magari yao.

Neutral wakati unasukuma Gari tuu, madhara huwezi kuyaona siku moja tu.
 
Huyu ametafuta kujitangaza uuzaj wa magari ila amechagua mlango mwembamba wa kujitumbukiza kwenye technical issues.
 
1. Kushuka kwenye mteremko gari ikiwa neutral, hii inasababisha kuzuia oil kusambaa na kusababisha msuguano kukosa kilainishi hicho na kupelekea kusagika kwa baadhi ya sehemu.

2. Kukanyaga mafuta kabla ya kubadilisha gear. Hii ni hasa kwa vijana unawasha gari na kuanza kupiga resi, kitendo hicho husababisha msuguano mkali na unaweza kuharibu sehemu za engine.

3. Kubadilisha gear wakati gari bado inatembea, hakikisha unakamata brake kwanza ndipo ubadilishe gear.

4. Kuweka neutral kweye taa nyekundu kwenye taa za barabarani, watu wengi hufanya hivyo ili kusave mafuta lakini kiasi unachosave ni kidogo sana kulinganisha na gharama ya tatizo unaloweza tengeneza, tumia brake ili gari liendelee kuwa kwenye drive mode, madhara hutokea unapoweka na kutoa neutral.

5. Kuweka parking kabla gari halijasimama kabisa. Hakikisha gari limesimama kabisa ndipo unaweka parking.

6. Kuendesha gari kwa speed ya juu kabla ya engine kupata joto, hasa kipindi cha baridi hakikisha engine imepata joto ili kuwezesha oil kusambaa kwenye sehemu zote.

7. Kuacha mafuta yakiwa machache katika tank, tank la mafuta linatakiwa kuwa full au kuwa nusu lakini sio chini kabisa. kuwa full kunasaidia engine na sehemu nyingine kuwa cool.

Imetolewa na Kimomwe Motors (T) Ltd, waagizaji wa magari. 0746267740

View attachment 1263795
hio namba 3 sijaielewa...
 
Yah, Hii inawezekana tu pale ambapo mafuta kwako Ni Kama mtaji wa garilo, yaani ukishajaza full tank ukifanya Safari ya Km kadhaa unaongezea mafuta kwa kadiri ulivyotumia gari siku hiyo ili kutoathiri mtiririko wa mafuta na utanikumbuka juu ya hili na utaenjoy Sana.
Full tank muda wote!!
 
Kwa mitelemko hii ya kwetu mi ni N mpaka nitakapopata mwinuko gari ina miaka 7 toka ninaliendesha mi hata ninasubili watu wavuke barabara kwenye taa kwenye gasia yoyote aah breki inatumika sana nawala sijaona tatizo kubadili oil mara kwa mara
 
Mkuu hiyo kitu hakuna tena gari za automatic ndio zimeundwa kuhimili hilo likitokea kwa bahati mbaya tofauti na gari za manual, nilishaona video gari mbili zilifanyiwa text auto na manual gari ya manual iliua kitu kwenye mfumo wa gear box na auto ilivumilia mshtuko huo.

NB: Sisemi ni jambo zuri kutoka R kwenda D, ila sio sahihi kusema kuwa kutoka N kwenda D kuna madhara yoyote kwa gari ya Automatic hata ikiwa kwenye motion. Nipo tayari kukusolewa kwa mwenye ufahamu zaidi
Dah...kwa gari yenye manual transmission haiwezekani kuingiza R wakati gari inaenda mbele....mfumo wake wa gia umelindwa kwamba R haiwezi kuingia Hadi gari isimame kabisa

Sent using Beretta ARX 160
 
Back
Top Bottom