Sawa mkuu! Wewe fanya lolote unalojisikia.Yan gari ni lako umenunua kwa pesa zako alafu bado waja wanakuchangaya nalo mara usifanye ivi mara vile...
Bro.. Kuna watu ni wabishi kwa asili yao. hivyo usitumie nguvu nyingi kumu elimisha MTU kama huyo utamaliza ugali wa bure.Kwani kuna mtu kasema usiweke full tank????
Sasa fundi mpaka gari imefika speed 180km/hr manake si ipo D automatically?au unadhan ipo gear gan kwenye auto unayoisemea?
Namba 3 sijaelewa
Hiyo namba saba ni sababu ya kiufundi au ya kibiashara? Maana kukeep engine cool, naomba ufafanuzi.
Nina maswali mawili:
1.Neutral gear inatakiwa kutumika wakati gani?
2.Madhara ya kuacha gari ikatembea na Petroli chini ya nusu tank au ikiwa tayari taa ya mafuta imewaka, tukiacha hilo ulilosema kuwa inasababisha engine kutokupoa vizuri? Ninauliza hivyo kwakuwa nimeshashuhudia Taxi au Daladala nyingi zikifanya hivyo vitu na sikuona madhara kwa hayo magari yao.
Kwa sasa zinaanzia 15m bossRafiki nje ya mada kidogo... Noah old model niandae shilingi ngapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
hio namba 3 sijaielewa...1. Kushuka kwenye mteremko gari ikiwa neutral, hii inasababisha kuzuia oil kusambaa na kusababisha msuguano kukosa kilainishi hicho na kupelekea kusagika kwa baadhi ya sehemu.
2. Kukanyaga mafuta kabla ya kubadilisha gear. Hii ni hasa kwa vijana unawasha gari na kuanza kupiga resi, kitendo hicho husababisha msuguano mkali na unaweza kuharibu sehemu za engine.
3. Kubadilisha gear wakati gari bado inatembea, hakikisha unakamata brake kwanza ndipo ubadilishe gear.
4. Kuweka neutral kweye taa nyekundu kwenye taa za barabarani, watu wengi hufanya hivyo ili kusave mafuta lakini kiasi unachosave ni kidogo sana kulinganisha na gharama ya tatizo unaloweza tengeneza, tumia brake ili gari liendelee kuwa kwenye drive mode, madhara hutokea unapoweka na kutoa neutral.
5. Kuweka parking kabla gari halijasimama kabisa. Hakikisha gari limesimama kabisa ndipo unaweka parking.
6. Kuendesha gari kwa speed ya juu kabla ya engine kupata joto, hasa kipindi cha baridi hakikisha engine imepata joto ili kuwezesha oil kusambaa kwenye sehemu zote.
7. Kuacha mafuta yakiwa machache katika tank, tank la mafuta linatakiwa kuwa full au kuwa nusu lakini sio chini kabisa. kuwa full kunasaidia engine na sehemu nyingine kuwa cool.
Imetolewa na Kimomwe Motors (T) Ltd, waagizaji wa magari. 0746267740
View attachment 1263795
Mkono mtupu haulambwi, jinyonge au mshtaki kama kafanya jinai. Kuna watu sijui mlizaliwa saa ngapi?Huyu ametafuta kujitangaza uuzaj wa magari ila amechagua mlango mwembamba wa kujitumbukiza kwenye technical issues.
Full tank muda wote!!
Nimecheka kwa sauti aiseeKuna gear sijawahi zitumia toka nijue kuendesha gari, Neutral, 2 na L. Mimi ni mguu kwenye break hata masaa matatu fresh tu.
Dah...kwa gari yenye manual transmission haiwezekani kuingiza R wakati gari inaenda mbele....mfumo wake wa gia umelindwa kwamba R haiwezi kuingia Hadi gari isimame kabisaMkuu hiyo kitu hakuna tena gari za automatic ndio zimeundwa kuhimili hilo likitokea kwa bahati mbaya tofauti na gari za manual, nilishaona video gari mbili zilifanyiwa text auto na manual gari ya manual iliua kitu kwenye mfumo wa gear box na auto ilivumilia mshtuko huo.
NB: Sisemi ni jambo zuri kutoka R kwenda D, ila sio sahihi kusema kuwa kutoka N kwenda D kuna madhara yoyote kwa gari ya Automatic hata ikiwa kwenye motion. Nipo tayari kukusolewa kwa mwenye ufahamu zaidi