Vitu vilivyopanda bei chini ya Uongozi wa Rais Samia

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,391
9,665
Hapa naweka baadhi tu ya vitu vilivgopanda Bei, bila kujali Vita ya Urusi. Vingine vilipanda tangu mwaka Jana.
1. Kuunganisha umeme.
2. Tozo za kutuma na kutoa hela
3. Mafuta ya kula
4. Umeme wa LUKU.
5. Nauli za usafiri.
6. Bei za vifaa vya ujenzi.
7. Mafuta ya Petrol/Diesel/ Taa.
8. Soda.
9. Bei ya Nafaka.
10. Bei ya Sabuni

Wengine mnaweza ongeza ili ujumbe uwafikie kwamba wanatakiwa wafanye kazi kwa makini na sio kusingizia vita na kuendelea kuandaa matamasha tu, kila siku Rais Yuko kwenye matamasha ili kumpotezea mda.

Tamasha la Royo Tuwa, Tamasha la Afya, Tamasha la Siasa, Tamasha la UVCCM, Tamasha la Wanahabari n.k

Tunataka kazi na maamuzi hata kwenye mambo Magumu.
 
Kama yupo sawa upstairs atatafuta immediate short term plan za ku-solve tatizo, au kama akiamua kuilaza akili yake aendelee kusema bei za vitu zitazidi kupanda.

Hayo majibu yake ni sawa na taifa halina kiongozi, na wala asijidanganye anasema ukweli, huko kusema kwake ukweli kwa waelewa ni sawa na anakiri akili yake imefika mwisho wa kutafakari.
 
Wewe kwenye sita kwa sita unakazana kuleta watoto Duniani kwa mawazo yako kua:
1. Elimu ni bure mpaka sekondari
2. Matibabu ni bureeeeee
Waamerika wana msemo wao " There is no free Lunch in Amerca"
Tafakari!!!!
 
Kama yupo sawa upstairs atatafuta immediate short term plan za ku-solve tatizo, au kama akiamua kuilaza akili yake aendelee kusema bei za vitu zitazidi kupanda.

Hayo majibu yake ni sawa na taifa halina kiongozi, na wala asijidanganye anasema ukweli, huko kusema kwake ukweli kwa waelewa ni sawa na anakiri akili yake imefika mwisho wa kutafakari.
Hebu pendekeza hapa hizo immediate short term plans ambazo wewe uliye smart upstairs unazijua
 
Gharama za ku gharamia deni la taifa; chini ya Magufuli deni lilikuwa maintained kwa wastani 7.5 billion dollars kwa miaka yote sita, bi tozo mwaka mmoja ameshakopa $2.5 billion na kufikisha deni karibu billion kumi huku makusanyo ya mapato yakiwa yameshuka.

Kazi ya upotoshaji wameachiwa wanasiasa mapashkuna wakiongozwa na Zitto Kabwe kusambaza uongo.
 
Hebu pendekeza hapa hizo immediate short term plans ambazo wewe uliye smart upstairs unazijua
1. Bunge likae kwa dharura, wafanye marekebisho kwenye bajeti, watafute pesa itakayosaidia kupunguza tatizo la uhaba wa mafuta mfano kupunguza/kufuta tozo za mafuta zilizopo kisheria.

2. Kupunguza matumizi ya anasa yasiyo ya lazima, mfano misafara ya viongozi kwa v8 , hizo pesa zikafidie pale ambapo makato ya tozo yatakuwa yamepunguza mapato.

3, Serikali itafute pesa za dharura, kama walivyoweza kutafuta za kucheza movie ya Royal Tour. Hizo pesa nazo ziingizwe kwenye gharama ya uagizwaji wa mafuta ili kuhakikisha mtu wa chini anapata nafuu kwenye bei ya mafuta, hapa serikali iwe msimamizi.

Au.

Watenge kiasi cha pesa ili kufidia makali ya bei ya mafuta kupanda, hili mfano wake ni kama serikali ya Kenya ilivyofanya.
 
Too extreme measures. Haziwezekani hizo options zote.

1. Unrealistic option. Kubadilisha bajeti ni kitu cha ajabu ambacho kitasababisha panic na uchumi kuyumba zaidi.

2. Austerity measures kwa Tanzania bado haziwezi kuleta pesa ya maana sana. Kwa kiwango cha kupanda kwa bei kilichopo, hii njia haina msaada.

3. Hakuna pesa za serikali zilizotumika kwenye Royal Tour. Ni pesa za matajiri wachache walijichanga wakampa ufadhili mama ili atengeneze hiyo movie yake na Peter.

Au.
Hii angalau. Japo haitashusha bei ya kila kitu. Kuna kaunafuu kataonekana lakini inflation bado itakuwa juu kwa sasa mpaka Urusi na Ukraine watakapokubaliana kuishi kwa urafiki.
 
Njia ya uhakika ni kupunguza kodi kwenye mafuta na hii itasaidia bidhaa nyingi kushuka bei na waondoe kodi mpya walizoweka ila tofauti na hapo tutaimba ngojera tu
 
Gharama za ku gharamia deni la taifa; chini ya Magufuli deni lilikuwa maintained kwa wastani 7.5 trillion dollars kwa miaka yote sita, bi tozo mwaka mmoja ameshakopa $2.5 trillion na kufikisha deni karibu trillion kumi huku makusanyo ya mapato yakiwa yameshuka.

Kazi ya upotoshaji wameachiwa wanasiasa mapashkuna wakiongozwa na Zitto Kabwe kusambaza uongo.

Kuna dhana hii inayosambazwa na hata Samia nae nimemsiskia akiieneza alipofanya mahojiano na Tido Mhando wa Azam kuhusu ukubwa wa deni la Taifa kukua kwa kasi lakini deni hilo LINAHIMILIKA; ingawa sasa nchi kikopeshwaji imekuwa na higher RISK kuliko hapo awali!!

Hii ni dhana potofu kwa ushamili wa nchi kwani nchi isilazimishe kukopa simply because deni linavumilika na wakopeshaji wako radhi kukopesha; nchi ilazimike kukopa pale tu inapokuwa ni lazima kukopa ili kuinusuru nchi na majanga yanayoweza kuikumba!!

Nchi isikope ili mradi kuna fedha za kukopeshwa kwani huo ni mzigo kwa vizazi vijavyo wakati huo wakopaji watakuwa wametoweka!!

Kwa serikali ya walamba asali dhana hii itawafanya wawe na matumizi ya hovyo kwani wanaamini kuwa wanakopesheka na tabia hiyo italiangamiza Taifa!!!
 
Kunadhana hii inayosambazwa na hata Samia nae nimemsiskia akiieneza alipofanya mahojiano na Tido Mhando wa Azam kuhusu ukubwa wa deni la Taifa kukua kwa kasi lakini deni hilo LINAHIMILIKA; ingawa sasa nchi kikopeshwaji imekuwa na higher RISK kuliko hapo awali!! Hii ni dhana potofu kwa ushamili wa nchi kwani nchi islazimishe kukopa simply because deni linavumilika na wakopeshaji wako radhi kukopesha; nchi ilazimike kukopa pale tu inapokuwa ni lazima kukopa ili kuinusuru nchi na majanga yanayoweza kuikumba!! Nchi isikope ili mradi kuna fedha za kukopeshwa kwani huo ni mzigo kwa vizazi vijavyo wakati huo wakopaji watakuwa wametoweka!!
6B086195-5C3E-4E7E-B89D-08789A6BF71B.jpeg

Kukopeshwa it’s not up to her administration willingness ata wakitaka, kuna shared appraisal report za ‘debt sustainability’ kutoka IMF and WB (kama hiyo abstract hapo from last September 2021).

In their role IMF/WB as global financial watchdogs wanatoa taarifa za wazi kuhusu uwezo wa nchi kulipa madeni in relation na makusanyo yake; pamoja na projection nyingine za kiuchumi.

Magufuli aliikuta nchi ipo kwenye moderate risks kwa miaka mingi ndani ya muda wa miaka mitatu aliishusha hadi low risk kwa kulipa madeni mengi ya watangulizi wake na kumaintain mkopo at $7.5 billion, bi tozo mwaka tu keshaongeza deni kufikia $9.5 billion; wakati mwenzake alikuwa anali manage at same threshold.

Ameongeza mkopo kuliko makusanyo, tumetolewa kwenye low risk tena na uwezi kupata mkopo wa bank kirahisi wenye interest za kibiashara if you are not low risks kwa hizi nchi za third world. Ndio maana akasema sasa hivi wataishi kwa concessional loans tu; ujue hapo IMF na WB washapiga beat.

Magufuli was special and jack of all trades including economy; bila ya hawa CCM kwenda kuomba radhi na kurudi kwenye njia zake alipoachia hii nchi wanaenda iharibu vibaya sana.

Watu wanaomtukana Magufuli wanamkosea sana sana he did nothing zaidi ya kutaka kuona nchi inapiga hatua. Na facts zipo sema tuwavivu tu kutafuta ukweli.
 
1. Bunge likae kwa dharura, wafanye marekebisho kwenye bajeti, watafute pesa itakayosaidia kupunguza tatizo la uhaba wa mafuta mfano kupunguza/kufuta tozo za mafuta zilizopo kisheria...
Hiyo no 1 mbona umeandika Kama mlevi au majnuni!!?..umezungukazunguka na kuchanganya Mambo,na no2&3 hazina tofauti yoyote na no 1!!..hawakujadili hii dharura bungeni juzi!!?..hapakua na hoja hii ya dharura!!?..unadhani bil 7 ya filamu inaweza kupunguza chochote kwenye Bei ya mafuta!?..msafara wa rais inagharimu kiasi gani,ni kiasi kinachotosha kubadili chochote kwenye kadhia ya mafuta!?..Kenya wamekopa imf ili
1. Bunge likae kwa dharura, wafanye marekebisho kwenye bajeti, watafute pesa itakayosaidia kupunguza tatizo la uhaba wa mafuta mfano kupunguza/kufuta tozo za mafuta zilizopo kisheria...
Hebu Soma no 1 kwa Makini uone umeandika vitu gani!?...hoja ya dharura haikuwepo juzi bungeni!?..Kenya wamekopa hela ya ruzuku imf,vipi unafunga mkono ukopaji Sasa?..msafara wa rais na filamu ni kiasi gani Cha pesa,kinatosha kutatuka suala la Bei za mafuta!?
 
Hiyo no 1 mbona umeandika Kama mlevi au majnuni!!?..umezungukazunguka na kuchanganya Mambo,na no2&3 hazina tofauti yoyote na no 1!!..hawakujadili hii dharura bungeni juzi!!?..hapakua na hoja hii ya dharura!!?..unadhani bil 7 ya filamu inaweza kupunguza chochote kwenye Bei ya mafuta!?..msafara wa rais inagharimu kiasi gani,ni kiasi kinachotosha kubadili chochote kwenye kadhia ya mafuta!?..Kenya wamekopa imf ili

Hebu Soma no 1 kwa Makini uone umeandika vitu gani!?...hoja ya dharura haikuwepo juzi bungeni!?..Kenya wamekopa hela ya ruzuku imf,vipi unafunga mkono ukopaji Sasa?..msafara wa rais na filamu ni kiasi gani Cha pesa,kinatosha kutatuka suala la Bei za mafuta!?
Tatizo la nyie chawa mnakera sana ipi ilikuwa hatua madhubuti kwa serikali kutoa tozo temporary ili kuondoa kupanda bei ya mafuta na kuzuia product inflation au kuwacha bei ya mafuta na kila kitu kipande serikali ichukiwe.

Ipo siku huyo maza kama anapita mitandaoni atagundua watu kama sisi tunaomkosoa ndio tulitaka afanikiwe kweli na watu kama nyie mnaendekeza matumbo yenu tu kwa kutetea mambo ya kijinga either yeye au wasaidizi yake wanafanya wakati results za mbele zinajulikana.
 
Hapa naweka baadhi tu ya vitu vilivgopanda Bei, bila kujali Vita ya Urusi. Vingine vilipanda tangu mwaka Jana.
1. Kuunganisha umeme.
2. Tozo za kutuma na kutoa hela
3. Mafuta ya kula
4. Umeme wa LUKU.
5. Nauli za usafiri.
6. Bei za vifaa vya ujenzi.
7. Mafuta ya Petrol/Diesel/ Taa.
8. Soda.
9. Bei ya Nafaka.
10. Bei ya Sabuni

Wengine mnaweza ongeza ili ujumbe uwafikie kwamba wanatakiwa wafanye kazi kwa makini na sio kusingizia vita na kuendelea kuandaa matamasha tu, kila siku Rais Yuko kwenye matamasha ili kumpotezea mda.

Tamasha la Royo Tuwa, Tamasha la Afya, Tamasha la Siasa, Tamasha la UVCCM, Tamasha la Wanahabari n.k

Tunataka kazi na maamuzi hata kwenye mambo Magumu.
2025 wala si mbali, wananchi tutakuwa na jambo letu kama CCM hawatoiba kura zetu....this is too much now. Wananchi tunataka tutatuliwe masuala yetu nyeti eti tunalazimishwa kuangalia na kuishangilia Royal Tour, why?
 
Back
Top Bottom