MtotoKautaka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2018
- 1,001
- 2,058
Kuna mwamba mmoja aligongwa na gari mfupa wa juu wa mkono uloconnect na bega ukachomoka kwenye socket yake sapot ikabak ni ngozi, misuli na tishu zingine.
Kwa bahati nzuri ile ajali ilitokea karibu na hospital ya wilaya na ma dokta walikuwa wapo nje wameenda kupata lunch. Wakawahi kumchek jamaa wakagundua kuwa mkono umechomoka kwasababu ulikuwa umelalia mgongoni kwahiyo ilikuwa ni rahisi kwa mtaalam kugundua.
Basi wakamuwahi kwa kushirikiana na wananchi walokuepo eneo la tukio wakamshikiria jamaa na kumfunga macho asione kinachoendelea madokta wakafanikiwa kuurejesha ule mkono.
After pale jamaa akapelekwa hospital akapewa dawa za maumivu na sapot ya mkono kwasababu alikuwa bado anahisi maumivu.
Kumbe ule mkono haukurudi vizuri kwenye njia zake kama ilivotakiwa jamaa akawa hawezi kuunyanyua mkono kuupeleka juu unaishia usawa wa kifua yani akiwa anainua mkono kama askari apigavyo kwata. Na pia kulikuwa na mfupa flani wa juu ya bega ulikuwa unauma pamoja na kwamba siku zilikuwa zishapita nyingi toka alipopata ajali.
Siku moja jamaa yupo mishe mishe sokoni akapita msela mmoja kabeba gunia la mpunga bagani akamgonga jamaa kwa nguvu bagani kwenye lilelile bega lenye shida. Alivogongwa lile bega likatoa mlio kama vile mifupa imehama flani jamaa anakwambia palepale yale maumivu ya bega yalokuwa yamebaki yakaondoka na akajaribu kunyanyua mkono akaona unaenda mpka mwisho. Badala ya kukasirika jamaa aliishia kumshukuru yule jamaa wa gunia kwa kumgonga begani na mpka saivi bega lipo safi kabisa na hama maumivu.
SO EVERYTHING HAPPENS FOR A REASON!!