Mi nadhani hii kitu inategemea na jinsi mlivyo na hatua ya uhusiano wenu...
Kuna watu hawajali sana umwambie usimwambie ni shauri yako, yaani wengine wanasema " tunapoanza na wewe ndio historia yetu inapoanzia, sitaki kujua huko nyuma umefanya nini na umepitia nini..."
Hivyo ni muhimu kumsoma mwenzio ni wa namna gani kabla ya kueleza au kumezea mambo ya historia yako...!
Kwa sisi wenye wivu huwa tunawashwa kutaka kujua mengi, matokeo yake ni "kuku ukimchunguza sana....... loh"
Lol
Umesema kweli mkuu!
Kama ni mpenzi tu ambae huna uhakika na mtakapofika unaweza ukalimit unayomwambia ili usije ukakuta mambo yako yanajulikana kila kona. . . Ila mkishaamua mnaingia ndoani na mipango ya kuwa na watoto ikiwepo kwakweli binafsi sioni kama kuna lakuficha maana mengi yanaweza yakaja mhusu mwenzio pia. Yawe ya kifamilia au binafsi.
kwakweli inategemea na mapenzi yenu yalivyo........
1.kuna mapenzi ,zaidi ya kuwa wapenzi mnakuwa marafiki sana na mnaelewana sana inafikia mahali you all confess to your past experience kiasi kwamba some you take them as jokes.
2.kuna mapenzi mtu anaona kuwa sasa your looking for the future na kila mmoja analake kifuani kwahiyo mtu anaona atoe tu kwa kadri atakavyoona yeye inafaa.
3.kuna wale ni wadadisi sana mko kwenye uhusiano unaulizwa maswali mengi sana ambayo inabidi uyajibu kwa kadri unavyoona inafaa kulingana na uelewa wa huyo mtu(ila ubaya wake uulizwe halafu udanganye siku aje kujua ukweli ,patachimbika sana)
4.kuna wale ambao si waelewaji kulingana na ulivyomsoma ,huwezi kumwambia hata hiyo kidogo.
5.kuna wale ambao ni too much open guy/lady yeye hukueleza tu ukweli no matter what will happen.