VITU AMBAVYO UKIVICHANGANYA LAZIMA KIMOJA KIFE/KIHARIBIKE.

thanks again and have you

JF-Expert Member
May 11, 2023
230
423
Habari za Jumapili ,!? Poleni na mihangaiko leo nimeamua niwaletee vitu viwili ambavyo ukivichanganya lazima kimoja kife /kiharibike.

.1KAZI NA UNDUGU.
Katika Maisha yetu ya Kila siku tusipende kuchanganya kazi na UNDUGU hasa kuwaweka ndugu zetu kutusaidia katika biashara au mradi binafsi kwa sababu ni ngumu kuwawajibisha nahapo unaweza haribu Biashara yako au ukiamua kuwawajibisha undugu wenu unaweza kuharibika.


2.BIASHARA NA URAFIKI.

Pili kuchanganya URAFIKI kwenye biashara si jambo zuri ,hasa tabia ya kukopeshana fedha ,kukopeshana bidhaa kwasababu urafiki wa kushibana Mara nyingi unaweza sababisha umuamini mtu na ushindwe kumchukulia hatua zaidi na endapo utamchukulia hatua urafiki wenu unaweza kuishia hapo.!

Nashukuru yangu ni hayo.
 
Back
Top Bottom