S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 82
Rais Kikwete atoa waraka wa mwisho kwa majamabazi
* Atangaza operesheni mpya, aonya serikali isije ikalaumiwa
Na Midraj Ibrahim, Muleba
Rais Jakaya Kikwete ametangaza rasmi kuanza upya operesheni ya kusaka majambazi nchini mwezi ujao.
Aliwataka majambazi kujisalimisha na wananchi wanaowaficha kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya operesheni kuanza.
Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Muleba jana, rais Kikwete alisema operesheni mpya haitajali mtu na hakutakuwa na huruma.
"Napenda kuwaarifu mwezi ujao tutaanza operesheni kubwa nchini ya kusaka majambazi," alisema Rais Kikwete na kuongeza akiseama : "mtalaumu sana, lakini mtajilaumu wenyewe kwa kuwa ujambazi unafanya binamu, mtoto wa mjomba, lakini mnawaficha, watoeni kabla operesheni hiyo haijaanza."
Rais Kikwete alisema tangu serikali yake iingie madarakani, hakuna jambo gumu lililowashinda na kwamba sasa watachukua hatua zinazotahili lakini serikali isije ikaluamiwa.
Alisema hivi sasa vumbi la majambazi limetulia, wakibuni mbinu mpya na kwamba, kabla hawajaibuka watateketezwa na salama yao ni kujisalimisha.
Akzungumzaia kuchelewa kukamila ujenzi wa wa barabara ya Kagoma-Lusahunga alisema watambana mkandarasi ili akamilishe kulingana na mkataba.
Alisema suala la ulinzi na usalama halina mjadala ni jukumu la serikali na aliwaahidi wananchi kuwa majambazi hawataachwa watambe.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo, Mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi, alimsifu Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kupambana na mafisadi wakubwa.
"Umeonyesha mfano, umeanza na mafisadi wakubwa wewe endelea, sisi tutawashughulikia hawa wa chini ili tukutane katikati, wewe endelea kaza uzi!" alisema Masilingi.
Masilingi alisema hawatakubali fedha za umma kufujwa na wachache na kuongeza kuwa watapambana nao, wakishindwa wataomba msaada ngazi za juu.
Akiwa wilaya ya Chato juzi, Rais Kikwete aliwashukuru wananchi kwa kumchagua John Magufuli ambaye alisema ni msaidizi wake muhimu kutokana na utendaji wake mzuri.