Abdul Ghafur
JF-Expert Member
- Sep 18, 2017
- 610
- 733
Wadau,
Wana Vitendo SACCOS wote na wote ambao bado hawajajiunga na Vitendo SACCOS...
Tunafuraha kuchukua fursa hii ya kuwakaribisha na kuwaalika nyote kuhudhuria mkutano wetu wa kawaida wa pili (wa kwanza ulikua tarehe 01/05/2017 kutangaza nia ya kuunda Vitendo SACCOS). Mkutano huo utakuwa na agenda kuu mbili, kwanza kutakuwa na semina itayotolewa na Afisa Ushirika Kibaha. Pili, tutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa muda.
Tunatarajia kuchagua Mwenyekiti, Katibu na bodi ya kwanza ya Vitendo SACCOS. Pia tutachagua Wana kamati wa kamati mbili za awali. Kamati ya usimamizi na kamati ya mikopo.
Kila mwana VTS ana haki ya kuwania nafasi hizo, ana haki ya kupendekeza mwana VTS yeyote, ana haki ya kupendekezwa na Mwana VTS yeyote.
Tunawakaribisha nyote katika mkutano huo utakaoanza saa tano kamili za asubuhi na kuendelea mpaka saa saba mchana. Uchaguzi huo utahudhuriwa na Afisa Ushirika wa Kibaha kuhakikisha unakuwa huru na unafata sheria na kanuni zote za vyama vya ushirika ya mwaka 2013.
Mkutano utafanyika tarehe 21/10/2017, Vitendo Cinema Hall, mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, Kibaha - Pwani.
Google Maps
Kwa wataohudhuria tafadhali wasiliana nasi kwa whatsapp 0625249605.
Asanteni sana.