thread hii imenigusa sana,ni kweli haya yanayozungumzwa huenda yanafanyika na ni vema kuchukua hatua kukabiliana na vitendo hivi vya kishenzi la sivyo watoto wetu wa kiume kwa wa kike watakuwa katika hatari ya kuharibiwa future yao au hata kuambukizwa magonjwa!
Wachangiaji mmechukua hatua gani kuondoa ili tatizo?
Wachangiaji mmechukua hatua gani kuondoa ili tatizo?
kwakweli ni aibu hivi wenye shule wao wapi au wakishadaka ada na mshiko wa usafiri wanajisahau na je wenye magari wanawajibika vipi kwa hili maana shule nyingi zinakodi magari
Story ya kutunga hii!
mHHHHHHHHHH KAMA KWELI NAMWAMISHA SHULE MWANANGU
Kuna habari moja niliisikia mwaka jana shule moja iko Upanga kama sikosei. Kuna mtoto wa kike alikuwa wa kwanza kuchukuliwa nyumbani , wa mwisho kurudishwa. Ikafika kipindi akawa anakataa kwenda shule asubuhi. Mama yake akawa anamgombeza sana, umeshakuwa mtoto mbaya wewe, unakataa shule kwa nini (Waafrika ndivyo tulivyo, hatuna muda wa kudadisi atoto we2). Basi mwalimu wa yule mtoto akawa ameobserve changes kwa kale kabinti, mtoto hakuwa na raha hata kidogo. Akapeleleza hakupata jibu. Siku moja akawapa watoto wote darasani kipande cha karatasi. Akawaambia kila m2 aandike asichokipenda. Basi wale watoto wakaanza kuandika. Wengine waliandika hawapendi uji, wengine kuoga, malaria etc. Lakini yule mtoto akaandika sipendi "School Bus"! Mwalimu akajiuliza ni kwa nini? Coz zoezi lote lilimtarget yule mtoto. Nadhani huyu mwalimu anafahamu vizuri saikolojia ya watoto.
Basi akamwita mzazi wa yule mtoto, wakaanza kumpeleleza, wakakuta mtoto keshaharibika siku nyingi! It was too late. Jamani tuwe na mazoea ya kuwahoji watoto wetu kuhusu vitu wasivyovipenda, na wanavyovipenda na tuwafwatilie kwa makini.
Hakuna faida ya kutafuta pesa wakati watoto wanaharibikiwa.
Wazazi wapeleke watoto wao shule wenyewe ni namna ya kujipanga tu hakuna kinachoshindikana.
watu wengine bwana mtu atunge story kwa maslahi ya nani humu ndani jamvini jaribu kuwa serious watu wanaongea vitu vinvyotokea mitaani
Tatizo lipo na ni kubwa.mara nyingi wenye mashule wana shauriwa waweka matroni mtu mzima badala ya konda wa kiume. kwa namna moja inapunguza tatizo.
hili suala ni la uzito na wazazi inabidi kuwa waangalifu sana. wazazi wenye watoto wapandao haya 'shool buses' inabidi kuwachunguza watoto wao katika maongezi na kupata kujua yote yanayojiri kwenye mabasi. Watoto hawadanganyi, ukiwapatia jinsi ya kuongea wanaongea vizuri.
......well subiri mtoto wako aje anajisiwe then hiyo itakuwa ya ukweli...hata mimi nakuunga mkono sawa eeeh?Story ya kutunga hii!