Vitambulisho vya Taifa vinakosa sifa za 'smart card'

Vitambulisho vya Taifa vinakosa sifa za 'smart card'

Unajua mimi simraumu JPM..

Maana nahisi baada ya kuona hayo mapungufu kwenye ID alitembelea ofisi za NIDA ili kuuliza.

Sasa hapa napata shida kidogo, inaonesha hata hao NIDA hawajui umuhimu wa hizo ID.
Maana Kama JPM angefunuliwa yote hayo sidhani kama angewashutumu NIDA kwa kiwango kile.

Ki ufupi hata hao NIDA wameshindwa kutoa elimu ya kutosha kwa muheshimiwa.
 
Kwa hiyo jpm Jana amekurupuka na yy kushangaaa hakuna signature ssa hivi hanaga washauri ,tukisema anajifungia mwenyewe anakuja kuongea hata asilojua kujifanya unajua kila kitu utaumbuka,namuonaga hata sefue akisoma mateuzi yake usoni hana Amani kabisa,kukumbusha ni kwamba nida tulipeleka mavyeti ya shule,ya kuzaliwa,maleseni ya magari na hata kadi za kura na walichukua muda kuhakiki taarifa.Sasa ile kadi ya lubuva tulienda bila id yoyote unaulizwa jina,ulipozaliwa mwaka na tarehe wanaingiza ktk database hivi nani hapo atakuwa na taarifa sahihi kama sio nida so jpm asimsifu lubuva kwa kuwa alimbeba aangalie ukweli sitetei matumizi mabaya ila facts tuziongee

Kiukweli pamoja na matumizi mabaya ya fedha(kama kweli wamekula wenyewe bila memo-externa drive) mambo mawili mkuu wa nchi amewalaumu NIDA:
1. Matumizi makubwa kwa quantity ndogo
2.Kitambulisho kukosa sahihi

Hayo mambo ya fedha ni ngumu hadi CAG aje aseme, au kama kuna mchepuko wa matumizi kwa maelekezo saga itaisha chinichini.

Kuhusu sahihi, kuna wadau wamesema kwenye nyuzi mbalimbali kuwa nchi nyingi sahihi haipo ila kuna finger prints na data ambazo ili uzi access lazima uwe linked na mtandao unaweza kujua details za ID owner. Sasa hapa kuna mawili,NIDA walishindwa kumfafanulia hasa National ID zinakuaje, au walimfafnulia hakuelewa au akaona wanaongea porojo au hakwenda kuomba kufafanuliwa, au kuna watu walimlisha maneno mh nae kwa kuwa anawaamini akajua hawa NIDA ni jipu. Hata hivyo pamoja na kwamba kuna minong'ono kuwa hawa NIDA officials wamepiga sna hela, ngoja vyombo vya dola vifanyekazi zake, kama kuna matumizi mabya ya madaraka na fedha sheria ichukue mkondo wake
 
Meta Stress Free Zone

Tusiwe washabiki wa mambo tusiyoyaelewa,tatizo lililopo ni kuwa uelewawa wa watanzania kuhusu national ID ni mdogo.Id haikutengenezwa kwa minajili ya kusomwa kama kadi zilizozoeleka mfano bima ya afya,voters ID.
National ID ina content ya taarifa zote za mwananchi na ni taarifa nyingi kuliko ID yeyote katika taifa letu.Kilichopo ili uweze kuziaccess taarifa za kitambulisho cha taifa ni lazima uwe umeunganishwa katika mfumo wa mamlaka hapo ndio unapata kitu kinaitwa wadau wa kitambulisho cha taifa mfano mabenki,tra,bodi ya mikopo na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kupata taarifa kwa matumizi mbali mbali.
Hivi sasa mabenki katika mkoa wa Dsm wanasisitiza kutumia national ID kwakuwa wameshapewa elimu,wameunganishwa na mfumo wameona umuhimu wa taarifa zilizopo ambapo biometric finger prints iliyomo ndani ya national ID ni feature kubwa zaidi ya signature ambayo mtu yeyote anaweza akaiguess iwapo kama sahihi ya nje ikiwa ndio kigezo.
Namba nne katika national ID ni mwaka wako wote na tarehe yake,
Inayofuatia mfano 12105 ni postcode ya eneo husika mfano tabata,namba zinazofuatia mfano 00004 ni namba yako katika mtaa husika kwa watu wenye Mwaka kama wako.namba mbili za mwisho ni unique namba ya mmiliki Wa ID.
Tatizo lililopo elimu haijatolewa ya kutosha ili watu wapate uelewa.
19841213121050000512 mfano Wa namba hiyo ndio kielelezo cha maelezo yaliyotolewa juu.
Kuhusu expire date inatumika ili kuja kuapdate taarifa za muombaji.
Kwakifupi naamini tutapata mwanga.

Ukiondoa hoja ya gharama ...HOJA ALIZOTUMIA RAIS MAGUFULI KUWAUMBUA NIDA NIMEGUNDUA BAADA YA KUJIELIMISHA...NI ZA KUKURUPUKA NA KUWA TAYARI AMESHAWAHUKUMU KINA MWAIMU.......LAKINI ANGETAKIWA KUONGELEA TU GHARAMA ...
KUHUSU GHARAMA PENGINE NI MAKOSA YA KIMKAKATI YAMEWATOKEA...INAWEZEKANA WALIWEKEZA PESA NYINGI KUJENGA INFRASTRUCTURE YA MTANDAO WA OFISI ZAO KUANZIA KATA .....AMBAPO WANGEWEZA KUTUMIA OFISI ZA WATENDAJI KATA KWA KUANZIA NA KUWEKA DAWATI LAO ....PENGINE WALIAJIRI WATUMISHI WENGI SANA ....NA KUNUNUA VIFAA BILA UUWIANO.......HII PENGINE NI UTAWALA WAO MBOVU ....SASA SIJUI KISHERIA .....
UNAWEZA UKAWAPELEKA MAHAKAMANI UKASHANGAA WANACHOMOKA
 
Kwa namna MAGUFULI alivyoongea Juzi.....Pamoja na kumuunga Mkono RAIS wangu...lakini naona tunayo safari Ndefu Sana .....ILE hotuba anayeweza kuishangilia NI Mtu ambaye hajaenda shule ....NI aibu KUWA hotuba ILE imetolewa Mbele ya Majaji ...ingetolewa pale Jangwani wala nisingeshsngaa
Kama RAIS kuna lugha stahiki kuongea Mbele ya kila hadhira .....Iwe kwenye kampeni,Mbele ya mabalozi, ( kwanza hadi Sasa hajaandaa state house cherry ..kusherekea mwaka mpya na mabalozi) ...Mbele ya wanasheria ...kuna maeneo hutegemewi kutoa hotuba kwa hisia ...PENGINE alikuwa na hotuba iliyoandaliwa ...namshauri kwenye formal events wasaidizi wake wahakikishe anasoma hotuba Yake .....hata marais wenye akili Kama Obama hawezi kuongea na Baadhi ya makundi bila kusoma hotuba.....maana kosa au sentensi moja tu UNAWEZA kuharibu kila kitu na ikawa scandal ..

Namshauri watu wa mawasiliano Ikulu wasitishe kuirusha ile hotuba ...maana inaenda Kuleta mjadala mkali Sana KUANZIA kwa Wasomi...na watu wa kawaida wanaweza kuelewa
 
Waweke Sigmature, DoB ili viwe kama NEC,DL wanaficha nini wakati wengine wameweka

DoB nimejaribu kuifafanua hapo nyuma ipo kama una national ID katika zile namba 20 unazoziona namba nane za kwanza ni mwaka wako mwezi wako na tarehe yako ya kuzaliwa.
Signature ni issue nyingine lakini kama unavyojua nchi yetu bado tuna lundo la watu wasiojua kusoma na kuandika so unaweza kuta ID zenye sahihi ni chache kuliko za wasiojua kusoma na kuandika.Je hilo litafanya ID ya wasiojua kusoma sio valid?kwakuwa haina signature?
Kwa wao NIDA taarifa haziosomwi kwa macho makavu zinasoma na mfumo kwa wadau husika maana lengo la ID ni kuwa ikufae pale unapohitaji huduma muhimu sio kuwa kama kitu cha kuonyesha tu,japo pia inakufaa kukutambulisha maana ina majina yako yote na security features kibao kama pesa.Ili upate uelewa mzuri jaribu tembelea bank yako kwa hapa Dar wao wamelimishwa na kuunganishwa katika mfumo technologia inayoitwa CIG ambayo taasisi husika zinasomana na database ya NIDA.
 
Meta Stress Free Zone

Tusiwe washabiki wa mambo tusiyoyaelewa,tatizo lililopo ni kuwa uelewawa wa watanzania kuhusu national ID ni mdogo.Id haikutengenezwa kwa minajili ya kusomwa kama kadi zilizozoeleka mfano bima ya afya,voters ID.
National ID ina content ya taarifa zote za mwananchi na ni taarifa nyingi kuliko ID yeyote katika taifa letu.Kilichopo ili uweze kuziaccess taarifa za kitambulisho cha taifa ni lazima uwe umeunganishwa katika mfumo wa mamlaka hapo ndio unapata kitu kinaitwa wadau wa kitambulisho cha taifa mfano mabenki,tra,bodi ya mikopo na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kupata taarifa kwa matumizi mbali mbali.
Hivi sasa mabenki katika mkoa wa Dsm wanasisitiza kutumia national ID kwakuwa wameshapewa elimu,wameunganishwa na mfumo wameona umuhimu wa taarifa zilizopo ambapo biometric finger prints iliyomo ndani ya national ID ni feature kubwa zaidi ya signature ambayo mtu yeyote anaweza akaiguess iwapo kama sahihi ya nje ikiwa ndio kigezo.
Namba nne katika national ID ni mwaka wako wote na tarehe yake,
Inayofuatia mfano 12105 ni postcode ya eneo husika mfano tabata,namba zinazofuatia mfano 00004 ni namba yako katika mtaa husika kwa watu wenye Mwaka kama wako.namba mbili za mwisho ni unique namba ya mmiliki Wa ID.
Tatizo lililopo elimu haijatolewa ya kutosha ili watu wapate uelewa.
19841213121050000512 mfano Wa namba hiyo ndio kielelezo cha maelezo yaliyotolewa juu.
Kuhusu expire date inatumika ili kuja kuapdate taarifa za muombaji.
Kwakifupi naamini tutapata mwanga.
Ni kweli mkuu unayonena..National ID za nchi nyingi zipo hivyo kimfumo
 
Nilipoona Rais anaongelea suala lile kwa mifano ya signature nilishangaa kweli nikahisi kuna walakini katika utendaji wake..anasikiliza zaidi wapambe kuliko wahusika wa kazi hiyo..Kwanini asingewauliza watu wa NIDA kabla ya kukurupuka na kudhalilika vile..Nahisi katika Wizara ambazo Mawaziri watachemka mapema ni hii ya Mambo ya Ndani nimeona walivyomshauri Rais vibaya kwenye Uhamiaji na NIDA
 
Kwa namna MAGUFULI alivyoongea Juzi.....Pamoja na kumuunga Mkono RAIS wangu...lakini naona tunayo safari Ndefu Sana .....ILE hotuba anayeweza kuishangilia NI Mtu ambaye hajaenda shule ....NI aibu KUWA hotuba ILE imetolewa Mbele ya Majaji ...ingetolewa pale Jangwani wala nisingeshsngaa
Kama RAIS kuna lugha stahiki kuongea Mbele ya kila hadhira .....Iwe kwenye kampeni,Mbele ya mabalozi, ( kwanza hadi Sasa hajaandaa state house cherry ..kusherekea mwaka mpya na mabalozi) ...Mbele ya wanasheria ...kuna maeneo hutegemewi kutoa hotuba kwa hisia ...PENGINE alikuwa na hotuba iliyoandaliwa ...namshauri kwenye formal events wasaidizi wake wahakikishe anasoma hotuba Yake .....hata marais wenye akili Kama Obama hawezi kuongea na Baadhi ya makundi bila kusoma hotuba.....maana kosa au sentensi moja tu UNAWEZA kuharibu kila kitu na ikawa scandal ..

Namshauri watu wa mawasiliano Ikulu wasitishe kuirusha ile hotuba ...maana inaenda Kuleta mjadala mkali Sana KUANZIA kwa Wasomi...na watu wa kawaida wanaweza kuelewa

Napingana na wewe. Hotuba ya Magufuli ilikuwa nzuri sana, tena sana. Amesema ukweli bila kuremba maneno. Tatito Watanzania tumezoea kusikia yale tunayotaka halafu kesho yake tunaanza kulalamika tumedanganywa. Ifike mahali mkuu wa nchi atueleze mambo kwa uwazi na ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu lakini walau tutakuwa tunajua ndio ukweli na tutafute tiba yake.

Ingekuwa hotuba ya Magufuli ni ya kuremba maneno kuna uwezekano watu wasingekuwa wanakumbuka karibu nusu kama si yote aliyoyasema. Lakini aliongea kama (a) Mtanzania anayeguswa na utendaji mbovu kwenye public sector na (b) kama kiongozi mwenye dhamana ya kurekebisha utendaji huo mbovu. Sasa hivi akichukua hatua wananchi wanajua where is coming from.

Nashawishika kusema watu wengi wanapinga hotuba ya Magufuli kwa sababu wana maslahi na mambo aliyotaja. Mfano hizo kesi 400 za wakwepa kodi!
 
Kwa kweli kasi ya raisi Magufuli kukurupuka imekuwa kubwa sana. Ubora wa kitambulisho cha taifa na mahitaji ya kidunia kwa sasa hakuna msomi anayeweza kutilia shaka. Labda gharama. Ila kikubwa pale ni mkono wa Membe kwa Mwaimu na uswahiba wao ndio umepelekea Magufuli atumbue jipu.

Wiki hii nimemkuta Dk Feisal aliyekuwa RAS Mwanza tukatangaziwa amefukuzwa kumbe hajafukuzwa bali amehamishiwa TAMISEMI Dodoma. Yupo Mkurugenzi wa Manisapaa ya Ilemela anaitwa John Wanga tulitangaziwa kasimamishwa kazi kwa ubadhilifu, jamaa yupo ofisini anadunda na jana alitokea ITV kwa tuhuma zingine za kuwadhulumu mgambo wa manispaa malipo yao ya kusimamia mitihani. Kama Dr Feisal na Wanga waliondolewa kwa kukurupuka unashangaa nini Magufuli kukurupukia sahihi ya kitambulisho cha taifa. Mzee anatafuta headlines tu wakati ana mamlaka yote kutawala
 
kimeandikwa national ID halafu kwa chini wakaandika CITIZEN ID
sasa hapo kimekaa vip wadau
 
Tuelewe pia National ID inatolewa kwa wakazi wote hata wasiokuwa raia. Ni Aibu msomi kuzungumza kutokea hewani-"no research no right to speak".
 
Mwaka wa kuzaliwa unaangali mwishoni mwa zile number nyingi nyingi kuna mwezi siku na mwaka kwa kifupi kipo poa..!!
 
Signature haiko viable kuliko fingerprints ,kwa ambao hamjapata hiko kitambulisho kina process kali mavyeti yote ya kuzaliwa na academic unayajaza na yanachunguzwa aisee
Hii ni komesha kwa wahamiaji halamu
 
Hizo id hazina shida, shida n kwamba zimetumika hela nyingi kwa id chache
hapa ndio niliuliza hivi katika zile gharama zilizotajwa zimetumika je ?
) gharama za wataalam wao zimo au hazimo? ?
2) gharama za kununulia mavifaaa yote zimo au hazimo?
3) gharama za kuanzisha majengo au kukodi ofisi ya ofisi zimo au hazimo?
4) gharama za shughuli ya usajili wwnyewe sasa ndio imo au haimo
5) gharama ya kununua hizo card imo au haimo
baada ya hapo tutoe zooote then tupate gharama ya ID sasa. hapo ndio tuone ukweli ukoje. NIDA WAJE WATUELEZEE vizuri tuelewe
 
Napingana na wewe. Hotuba ya Magufuli ilikuwa nzuri sana, tena sana. Amesema ukweli bila kuremba maneno. Tatito Watanzania tumezoea kusikia yale tunayotaka halafu kesho yake tunaanza kulalamika tumedanganywa. Ifike mahali mkuu wa nchi atueleze mambo kwa uwazi na ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu lakini walau tutakuwa tunajua ndio ukweli na tutafute tiba yake.

Ingekuwa hotuba ya Magufuli ni ya kuremba maneno kuna uwezekano watu wasingekuwa wanakumbuka karibu nusu kama si yote aliyoyasema. Lakini aliongea kama (a) Mtanzania anayeguswa na utendaji mbovu kwenye public sector na (b) kama kiongozi mwenye dhamana ya kurekebisha utendaji huo mbovu. Sasa hivi akichukua hatua wananchi wanajua where is coming from.

Nashawishika kusema watu wengi wanapinga hotuba ya Magufuli kwa sababu wana maslahi na mambo aliyotaja. Mfano hizo kesi 400 za wakwepa kodi!

HEKIMA KWANZA;
Laiti kweli ungekuwa na hekima kwanza. Hivi weye hukuona kuwa JPM alikuwa anahalalisha jipu lake alilotumbua kule NIDA? Alikuwa anataka asiseme alikosea kumtumbua Maimu tu. Hivyo vitambulisho hata kama vilikuwa vimetengenezwa na "Fala" asingekuwa mjinga kiasi hicho awe amekula mihela yoote hiyo, awe amewapa wakuu vitambulisho vyao, halafu nao wasione hizo hitilafu zote.
Kuhusu kesi za mihela lukuki, kuiambia mahakama ifanye chap chap ili awape robo ya hiyo mihela, NASEMA; Alikosea. Hukumu ikiharakishwa bila uangalizi nayo ni haki ilio uliawa. Hatutaki ichukue miaka, ila isiwe fasta. Itaua haki za watu. Je, ikijagundulika baadaye kuwa haki haikutendeka kama ile issue ya meli za samaki wa magufuli, hiyo hasara itabebwa na nani??
Aiache mahakama itende haki kwani ndo chombo pekee tunacho tumainia.
 
mahakama nazo zisiweke mazingira ya rushwa. kila kukicha kesi zinaahirishwa kwa sababu za kitoto sana! huu ni uzembe na kuandaa mazingira ya rushwa
 
mahakama nazo zisiweke mazingira ya rushwa. kila kukicha kesi zinaahirishwa kwa sababu za kitoto sana! huu ni uzembe na kuandaa mazingira ya rushwa

Kesi zikifyatuliwa hukumu za fasta hapo ndo rushwa italiwa kisawasawa kwani hakimu atategemea rufaa ikuokoe
 
Mimi ni mmoja wa Watanzania mwenye kitambulisho cha taifa ambaye hotuba ya Rais jana kufungua mwaka wa Mahakama imenigusa. Nimekiangalia kwa umskini, kinakosa sifa zote za "smart card" kama ifuatavyo:
1) Hakina nembo ya siri kama vike vya "road licence" na "kupiga kura".
2) Hakina mwaka wangu wa kuzaliwa kuthibitisha nina unri gani mimi Mtanzania.
3) Hakina sahihi yangu kuthibitisha hiyo picha na mimi niliye nayo ni changu.
4) Kina mwaka wa kikomo kwamba mimi Utabzania wangu utakoma hiyo siku hadi niombe upya!!!

TUTAFAKARI TUCHUKUE HATUA
Hata benki za Manzese hazikitambui,mwaka wako wa kuzaliwa upo ndio code ya kitambulisho chako anagalia zile namba za kitambulisho chako zinaonyesha siku,mwezi na mwaka uliozaliwa zimeunganishwa kwapamoja,mengineyote uliyosema ni kweli
 
Back
Top Bottom