Vitambulisho vya Taifa vinakosa sifa za 'smart card'

Vitambulisho vya Taifa vinakosa sifa za 'smart card'

Hata benki za Manzese hazikitambui,mwaka wako wa kuzaliwa upo ndio code ya kitambulisho chako anagalia zile namba za kitambulisho chako zinaonyesha siku,mwezi na mwaka uliozaliwa zimeunganishwa kwapamoja,mengineyote uliyosema ni kweli
Hahaaa muwe mnafanya research kwanza kabla hamjacomment pumba hapa, nembo ziko nyingi tuu ila kwa kukurupuka kwenu hamuwezi kuziona, chunguza National ID za dunia nzima ni lazima ziwe na deadline ili kuapdate taarifa, hayo mabenki yako ya manzese ndo hayatumii kwasababu wewe ni mkurugenzi kilaza, benki nyingine zoote zinavitumia kwasababu zinaelewa umuhimu na matumizi yake, wewe endelea kupiga kelele zisizo na research kama babu yako Magu
 
Mr Raisi JPM hakukurupuka na hotuba yake ni mahali pake kwa kuwa hii mambo ya kuandikiwa hotuba na kuficha mambo ndio imetufikisha kwenye hii hali ya kiongozi kujiona kuwa mungu mtu.Kuhusu NIDA ni wazi kuwa lengo lao bado ni zuri ila walihitajika kuwa na watu wanaoweza kujenga hoja na kuitetea kulingana na technolojia iliyotumika.Maana yake ni kwamba gharama iliyotumika pengine itakuwa robo tu ya mpango mzima wa vitambulisho nchi nzima kwa kuwa ID hii inabeba taarifa zote za raia,kama mdau alivyoainisha hapo juu lakini pia kuna taarifa ambazo ni biometric ambazo ni za muhimu zaidi kuliko sahihi yako zinazoonekana kwa kutumia card reader.Hizi taarifa muhimu ni pamoja na alama za vidole,rangi ya ngozi na macho,na mwisho sahihi yako ambayo inathibitisha kuwa taarifa hizo ulizozitoa ni za kwako na sahihi.Hizi ndio zinazotumiwa na idara nyingine kama uhamiaji,polisi TRA na kadharika.Kwa kuwa ID hii ndiyo inayotakiwa kuwa kama mfumo mama,mifumo mingine yote inatakiwa kuwa na uwezo wa kuingiliana na huu mfumo mkuu ili kupata taarifa na hapa ina maana ya kupata software itakayotekeleza hayo. Nilichogundua ni kuwa NIDA ina watendaji ambao wengi wao hajui uwezo wa utendaji wa ID wanazozitoa,Ni wachache sana wanauwezo wa kukueleze kinachoendelea ukaelewa vizuri,wengi wao wanachukulia kama kitambulisho cha kawaida pasipokufahamu upana wa matumizi yake.Mfano mdogo tu,hivi karibuni kuna officer hakujua kama kuna aina tatu za hizi ID zinazopaswa kutolewa.Mpaka watanzania wote wapate IDs kuna uwezekano gharama zikafikia billion 450.
 
Kwa namna MAGUFULI alivyoongea Juzi.....Pamoja na kumuunga Mkono RAIS wangu...lakini naona tunayo safari Ndefu Sana .....ILE hotuba anayeweza kuishangilia NI Mtu ambaye hajaenda shule ....NI aibu KUWA hotuba ILE imetolewa Mbele ya Majaji ...ingetolewa pale Jangwani wala nisingeshsngaa
Kama RAIS kuna lugha stahiki kuongea Mbele ya kila hadhira .....Iwe kwenye kampeni,Mbele ya mabalozi, ( kwanza hadi Sasa hajaandaa state house cherry ..kusherekea mwaka mpya na mabalozi) ...Mbele ya wanasheria ...kuna maeneo hutegemewi kutoa hotuba kwa hisia ...PENGINE alikuwa na hotuba iliyoandaliwa ...namshauri kwenye formal events wasaidizi wake wahakikishe anasoma hotuba Yake .....hata marais wenye akili Kama Obama hawezi kuongea na Baadhi ya makundi bila kusoma hotuba.....maana kosa au sentensi moja tu UNAWEZA kuharibu kila kitu na ikawa scandal ..

Namshauri watu wa mawasiliano Ikulu wasitishe kuirusha ile hotuba ...maana inaenda Kuleta mjadala mkali Sana KUANZIA kwa Wasomi...na watu wa kawaida wanaweza kuelewa

Achana nao sikio la kufa hao.
 
Pombe bwana...kaingia chaka hapo kwenye signature...lakin kwakweli hotuba yake nimeipenda sana
 
Ukiondoa hoja ya gharama ...HOJA ALIZOTUMIA RAIS MAGUFULI KUWAUMBUA NIDA NIMEGUNDUA BAADA YA KUJIELIMISHA...NI ZA KUKURUPUKA NA KUWA TAYARI AMESHAWAHUKUMU KINA MWAIMU.......LAKINI ANGETAKIWA KUONGELEA TU GHARAMA ...
KUHUSU GHARAMA PENGINE NI MAKOSA YA KIMKAKATI YAMEWATOKEA...INAWEZEKANA WALIWEKEZA PESA NYINGI KUJENGA INFRASTRUCTURE YA MTANDAO WA OFISI ZAO KUANZIA KATA .....AMBAPO WANGEWEZA KUTUMIA OFISI ZA WATENDAJI KATA KWA KUANZIA NA KUWEKA DAWATI LAO ....PENGINE WALIAJIRI WATUMISHI WENGI SANA ....NA KUNUNUA VIFAA BILA UUWIANO.......HII PENGINE NI UTAWALA WAO MBOVU ....SASA SIJUI KISHERIA .....
UNAWEZA UKAWAPELEKA MAHAKAMANI UKASHANGAA WANACHOMOKA
Rais naamini yuko very well informed, na hasa kama Rais mhusika ni mfuatiliaji wa mambo, so naamini amepewa taarifa za kutosha na hopefully NIDA wanaitwa kufanya clarification. Lakini siku zote kama kwenye organization hamjajipanga mtajikanyaga tuu huyu atasema hili yule lile na mwisho wa siku mtajichanganya tuu. Halafu mimi nimepita sana mikoani na mawilayani sijawahi ona ofisi zao let alone ngazi ya kata?
 
Hili la NIDA Mzee mtumbua vipele kachemka mno. Eti anashangaa hakuna sahihi? Teh, subirini aibu yaja.
 
Tarehe ya kuzaliwa IPO kwenye naomba za mwanzo za vitambulisho kuexpire ni kawaida ili utengenezewe kingine kulingana na technojia ya kipindi hicho
Kweli mkuu hata Mimi nimeona tar yangu ya kuzaliwa tatizo mtu badala ya kuuliza anapiga tu makelele
 
Habari za leo. Kuna uelewa mkubwa umekosekana kuhusu vitambulisho vya taifa. Raisi tayari aliagiza wakaguzi ikiwemo tume ya kuzuia rushwa kufanya kazi zao. Hivyo anasubiri taarifa. Naona yeye kuanza kuelezea amekosea. Aviamini vyombo vyake vimpe taarifa sahihi. Pili kuna audit ya value for money asubiri aletewe. Tatu kuhusu kitambulisho kukosa sahihi ilipaswa kutolewa taarifa na watu wa mamlaka husika wajieleze kwa nini viko hivyo, na ni swala ambalo ni purely professional.ikumbukwe kwamba Nida wana tuzo ya vitambulisho bora Afrika. Sioni mantiki ya kutaka vifanane na vingine kama kadi ya kura. Vilevile huwezi kulinganisha kitambulisho cha taifa na kadi ya kura. Ukusanyaji wa taarifa na zoezi zima ni tofauti. Kadi ya kura unapata ndani ya dakika kumi. Kitambulisho ujiandikishe uhojiwiwe na maafisa wa rita na uhamiaji wathibitishe taarifa mpaka kufikia production process inachukua muda na utapata kama umequalify. Ifahamike ukimsajili mtu kuwa raia unempa haki zote hadi kugombea uraisi. Ni zoezi makini sana magaidi wasije wakasajiliwa. As well as other related risks. Hivyobasi kurahisisha zoezi hilo ni hatari kwa usalama wa nchi
 
Uwepo wa signature kwenye ID haina mantiki kabisa maana bank wanaruhusu uwe na signature tofauti na ile ya kitambulisho.....
Bado hii ID ni nzuri
 
Michango yenu imefafanua halisi ya "Kitambulisho cha Taifa". Swali la msingi ni madhumuni na matumizi ya hicho kitambulisho. Kama taarifa zilizomo kwenye kitambulisho hicho lazima kiingizwe kwenye mtandao ndo zionekane, kwa matumizi ya kawaida, nchini kwetu, kinakosa hizo sifa.
 
Kwa namna MAGUFULI alivyoongea Juzi.....Pamoja na kumuunga Mkono RAIS wangu...lakini naona tunayo safari Ndefu Sana .....ILE hotuba anayeweza kuishangilia NI Mtu ambaye hajaenda shule ....NI aibu KUWA hotuba ILE imetolewa Mbele ya Majaji ...ingetolewa pale Jangwani wala nisingeshsngaa
Kama RAIS kuna lugha stahiki kuongea Mbele ya kila hadhira .....Iwe kwenye kampeni,Mbele ya mabalozi, ( kwanza hadi Sasa hajaandaa state house cherry ..kusherekea mwaka mpya na mabalozi) ...Mbele ya wanasheria ...kuna maeneo hutegemewi kutoa hotuba kwa hisia ...PENGINE alikuwa na hotuba iliyoandaliwa ...namshauri kwenye formal events wasaidizi wake wahakikishe anasoma hotuba Yake .....hata marais wenye akili Kama Obama hawezi kuongea na Baadhi ya makundi bila kusoma hotuba.....maana kosa au sentensi moja tu UNAWEZA kuharibu kila kitu na ikawa scandal ..

Namshauri watu wa mawasiliano Ikulu wasitishe kuirusha ile hotuba ...maana inaenda Kuleta mjadala mkali Sana KUANZIA kwa Wasomi...na watu wa kawaida wanaweza kuelewa

Lawama kisa sahihi, serious?

Pamoja na watu kufikiri NIDA ni watu walio na harufu ya kujilimbikizia mali, lakini hadi CAG na wakaguzi wathibitishe, na siyo hisia na maneno ya kuambiwa. Na unaweza kushangaa jamaa wakachomoka mahakamani
 
TUTAMBUE HILI:
National ID ya Tanzania si lazima ifanane na ID za nchi nyingine coz ID hiyo niya Tanzania na si ya nchi nyingine.

Kuweka sahihi zetu, Sura, ID Number, Finger Prints na vitu vingine ni mapendekezo ya wahusika dhidi ya utaalamu unaoendana na utafiti waloufanya.

Kwa mataifa makubwa wao wana DATABASE ya raia nchi nzima na anuani ya kila mmoja anapoishi na full information zake, so wao kuamua kuweka vitu vichache kwny National ID ni upendeleo wao kulingana na jinsi walivyojipanga kiteknolojia.

Kwa mataifa makubwa, ukifanyka uhalifu wanaenda eneo la tukio wanachukuwa alama za vidole kitaalamu mwisho wa cku wakiziingiza kwny computer wanapata taarifa zote za muhusika.

Tanzania ni vyema tukaweka picha coz bado hatuko vizuri kiteknolojia na pia lazma tuangalie mambo kwa faida yetu na si kwasababu Marekani wamefanya vile basi ni lazima nasi tuige kila kitu.

Kama zoez lilifanyka kifisadi bas lirudiwe kisha tukamilishe vigezo tunavyohitaji kuwanavyo ktk vitambulisho vyetu kulingana na uchumi wetu, uwezo wetu kiteknolojia na mengineyo.
 
Ndiyo issue ya Kwanza JPM kuni disappoint.
National ID si lazima kuwa ni signature. Data zote zipo kwenye database.
Siku hizi NMB ukitoa National ID unafungua account immediately na kupata ATM card maana wana uhakika na data zako hawahitaji tena barua ya serikali ya mtaa.
Lakini upande wa matumizi ya pesa na idadi ya vitambulisho JPM yupo sahihi. Haviendani kabisa
Si lazima lakn kwa Tz inaweza kuwa lazima kulingana na mazingira yetu.

Nchi nyingine zina teknolojia kubwa sana so hawana haja ya kuweka vitu vingi wakat wanauwezo wa kupata taarifa zako zote kwa muda mfupi.
 
Napingana na wewe. Hotuba ya Magufuli ilikuwa nzuri sana, tena sana. Amesema ukweli bila kuremba maneno. Tatito Watanzania tumezoea kusikia yale tunayotaka halafu kesho yake tunaanza kulalamika tumedanganywa. Ifike mahali mkuu wa nchi atueleze mambo kwa uwazi na ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu lakini walau tutakuwa tunajua ndio ukweli na tutafute tiba yake.

Ingekuwa hotuba ya Magufuli ni ya kuremba maneno kuna uwezekano watu wasingekuwa wanakumbuka karibu nusu kama si yote aliyoyasema. Lakini aliongea kama (a) Mtanzania anayeguswa na utendaji mbovu kwenye public sector na (b) kama kiongozi mwenye dhamana ya kurekebisha utendaji huo mbovu. Sasa hivi akichukua hatua wananchi wanajua where is coming from.

Nashawishika kusema watu wengi wanapinga hotuba ya Magufuli kwa sababu wana maslahi na mambo aliyotaja. Mfano hizo kesi 400 za wakwepa kodi!
Sijui tupewe Rais gani tumwone anatufaa hapa Tz. Tumepata kiongozi mzuri sana lakn cjui jaman aaah huwa nashindwa kusema. Mungu atupe nini sisi Watz. . . . . !!!
 
Michango yenu imefafanua halisi ya "Kitambulisho cha Taifa". Swali la msingi ni madhumuni na matumizi ya hicho kitambulisho. Kama taarifa zilizomo kwenye kitambulisho hicho lazima kiingizwe kwenye mtandao ndo zionekane, kwa matumizi ya kawaida, nchini kwetu, kinakosa hizo sifa.
Mkuu hapa umenena, swala la sahihi ni uamuzi na mapendekezo ya taifa husika, si.lazma walivyofanya marekani basi nasi tuwaige kila kitu.
 
Hamna cha Magufuli kukurupuka wala nini!! Pesa zimeliwa huyoo Mwaimu ana mshahara gani wa kuweza kununua mtaa mzima hapo nyuma ya shoppers plaza?? msitetee ujinga wakati wizi wa waziwazi unaonekana??? NIDA ilijaa wezi sanaa!!
 
Hahaaa muwe mnafanya research kwanza kabla hamjacomment pumba hapa, nembo ziko nyingi tuu ila kwa kukurupuka kwenu hamuwezi kuziona, chunguza National ID za dunia nzima ni lazima ziwe na deadline ili kuapdate taarifa, hayo mabenki yako ya manzese ndo hayatumii kwasababu wewe ni mkurugenzi kilaza, benki nyingine zoote zinavitumia kwasababu zinaelewa umuhimu na matumizi yake, wewe endelea kupiga kelele zisizo na research kama babu yako Magu
Wakati mwingine nashindwa kuelewa kama mtu anajua anachokisema,hicho kitambulkisho cha Taifa kinakataliwa na Benki nyingi tu ,kilitakiwa kiwe na Barcode au memory chip,na hakina vyote hivyo sasa hata ukiswap kwenye mashineza utambulisho, hakitatoa matokeo yoyote,wakati mwingine ni busara kukaa kimya kuliko kutoa maoni ya kitu usichokijua,mwishowe unaonekana MPUMBAVU.
 
Tarehe ya kuzaliwa,mwaka,na mwezi vipo kwenye kitambulisho tarakimu zake zimeunganishwa kwa pamoja
 
Hizo id hazina shida, shida n kwamba zimetumika hela nyingi kwa id chache
Basi tungejikita huko na siyo kujazia nyama kwamba havina viwango ili tupate support..mtu anayetaka kuona signature anunue cardreader..au umwombe kitambulisho cha bima ya afya uone signature
 
Waweke Sigmature, DoB ili viwe kama NEC,DL wanaficha nini wakati wengine wameweka
Kwani unaogopa utakuwa umesahau tarehe ya kuzaliwa? Tuweke signature kwenye certificate za shule tunaogopa nn? Mwuulize trafic ile signature kwenye DL inamsaidia nn? Sikia jibu lake harafu uone kama ina add value.
 
Back
Top Bottom