Vitambulisho vya machinga vipya vinatoka lini?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,037
9,953
December 10, 2018 Rais alizindua vitambulisho vya wajasiriamali na wachuuzi wadogo wadogo maarufu kama wamachinga na alisema vitadumu kwa mwaka mmoja, sasa mwaka umeisha na wachuuzi hawa wanahangaika kutafuta vitambulisho vipya na hakuna majibu yanayoeleweka.

Maeneo mengine tayari wachuuzi hawa wameshaanza kubananishwa kwa madai muda wa vitambulisho hivyo umeisha na hawajui wapi wataanzia kulalamika kwani kuna maeneo ya mitaa na vijiji hata viongozi waliochaguliwa hawajulikani kwani walipita bila kupingwa.

Hili lisipopatiwa ufumbuzi upo uwezekano kuzusha migogoro isiyokuwa na msingi kati ya serikali na wachuuzi machinga na wajasiliamali, kwani kuna maeneo wananchi wameanza kutozwa elfu 30 kwa madai Rais kapandisha bei jambo linajojenga taswira ya ubabaishaji serikalini.
 
Mku sasa hapo kazi ipo. Maana sehemu zingine wenyeviti waliopita bila kupingwa eti wananchi wa sehemu hizo hawawatambui sasa hapo wataanzaje kwenda kudai vitambulisho vipya? Mimi nafikiri sasa watangaze kuwatambua rasmi.
 
Akiishiwa pesa tu atarudi tena kuwachangisha! Sasa hivi anakomaa na mashirika kurejesha "fungi LA kumi"
 
Dah hivi vidude hata uko serikali za mitaa hawana majibu.
Waafrica hatupo serious na maisha
 
Back
Top Bottom