Serikali kuja na Vitambulisho vipya kwa Machinga vitakavyodumu zaidi ya mwaka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,236
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo katika mchakato wa kutoa vitambulisho vipya vya wafanyabiashara wadogo.

Mtendaji mkuu huyo wa shughuli za Serikali ameagiza machinga kutosumbuliwa katika biashara zao huku akiwataka wajasiriamali hao kutotumika na wafanyabiashara wakubwa kuuza bidhaa mitaani kwa kuwa kitendo hicho huchangia kukwepa kulipa kodi.

Majaliwa ameeleza hayo leo Alhamisi Januari 28, 2021 katika ufunguzi wa kongamano la mashauriano na machinga jijini Dar es Salaam.

Amesema vitambulisho vinavyoandaliwa vitakuwa na taarifa za ziada ikilinganishwa na vya awali vilivyokuwa vinatolewa kwa Sh20,000 na kwamba vitadumu zaidi ya mwaka mmoja.

“Mwaka jana Serikali ilianza kutoa vitambulisho na itaendelea kuvitoa ili kuwezesha kufanya biashara zao bila usumbufu. Serikali inaandaa vitambulisho bora zaidi vitakavyomtambulisha machinga mwenyewe na kutambulika katika mifumo mingine, itaondoa utaratibu wa vitambulisho vya sasa.”

“Kama tumeweza kufanikisha ubora wa vitambulisho vya Taifa, leseni tutashindwa nini vitambulisho vya machinga? Watalaamu watajadiliana na kutueleza na vitakuwa na ukomo zaidi ya mwaka mmoja,” amesema.

Katika ufafanuzi wake, Majaliwa amesema Machinga ni kundi muhimu linalorahisisha upatikanaji wa bidhaa nchini, kuchochea kujiajiri, kuchochea ukuaji wa pato la Taifa na kupunguza umaskini nchini.

Kongamano hilo la machinga kutoka mikoa 26 nchini limehusisha mfuko wa NSSF, huduma za bima ya afya na taasisi za kifedha zilizoeleza mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa urahisi zaidi kupitia vikundi badala ya mkopo binafsi.
 
Naanza kuhisi categories za wamachinga kwenye vitambulisho vipya.
 
Kwahiyo vitambulisho vya sasa serikali itatoa na risiti halafu ndo tunaambiwa pia vitatumika kukopea bank mikopo, na wakati wa kampeni tuliambiwa siyo lazima, @5 tena tutafika tu.
 
Itakuwa kuna namna maana jana watendaji walikuwa wanapita huku mtaani wakichukua taarifa za kila mfanyabiashara mpaka wale wamama wauza mihogo kwenye vindoo.

Mimi pia walinipitia wakachukua taarifa zangu japo niliwapa za uongo.
 
Sawa sawa Kwa hiyo kila mwaka kitambulisho kitalipiwa. Mkimaliza hao itakuwa zamu ya wafanyabiashara wakubwa. Vipi wajasiriamali nao kama vile wauza kuku, watengeneza pilipili n.k Chama oyeee
 
Walipe tu! Tena ikiwezekana wawaongezee na kufikia walau hata elfu 50 au laki 1 kabisa kwaa mwaka! ili hizo fedha zikanunulie meli za kisasa za uvuvi wa bahari kuu, na pia kununulia zile ndege zetu kubwa za mizigo.

Watumishi wa umma tumenyimwa stahiki zetu kwa zaidi ya miaka mitano sasa kwa kigezo kwamba hizo fedha zinakwenda kununulia Bombardier! Na bado kila mwezi tunakatwa kodi (Payee) iliyo changamka kweli kweli!

Hivyo siyo dhambi kwa kila mtu kulipa kodi anayo stahili.
 
Hivi mmachinga ataendelea kubaki mmachinga miaka yote? Hakuna namna labda mwaka huu alikua mmachinga baada ya miaka miwili naye awe na tin na atambulike kama mfanyabiashara anayeendelea kidogo ?
 
Jiwe aliahidi kwenye kampeni kwamba atatengeneza mabilionea wapya.

Naona ndiyo hao anawaandalia vitambulisho. Na Jana walikutana na pm

Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea
 
Jiwe aliahidi kwenye kampeni kwamba atatengeneza mabilionea wapya.

Naona ndiyo hao anawaandalia vitambulisho. Na Jana walikutana na pm

Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea
We kwa akili yako ulnashaur iweje,? Usitoe malalamiko bila solutions
 
Mitano tena !

Jiwe ashasema huwa hashauriwi Wala hawapangiwi. Akaongeza kwa kusema kuwa ukimpangia ndiyo unaharibu kqbisa!
Sasa hatakama alisema hvo mbn hajakosea, Kwan kulipa 20tsh kwa mwaka au Zaid n tatzo? Au hutak machinga walipe Kodi hata kdg? Mbn Mo Dewj haliilii et Kodi ila watoa buku kadhaa maneno mengiii😂😂
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom