Vitambulisho vya Askari kuorodheshwa, hili limekaaje?

Vitambulisho vya Askari kuorodheshwa, hili limekaaje?

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Zipo taarifa zisizotiliwa shaka kwamba waajiriwa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, katika kambi mbalimbali nchini, wametakiwa wakabidhi kadi zao za kupigia kura katika ofisi zao ili waweze "kuandikishwa".

Haya yameripotiwa Mara na mikoa mingine nchini. Mfano wa karibuni kabisa ni wa Polisi Mkoa wa Pwani ambako Tangazo limetolewa na Kamanda aliyejitambulisha kuwa ni Hamza (ASP).

Baadhi ya waajiriwa hawa wanahoji iweje kadi zao ambazo ni haki yao ya Kikatiba, ziorodheshwe na wakubwa? Wengine wanasema huenda uamuzi huo unatokana na ukweli kwamba wakati wa upigaji kura watakuwa wamesambazwa katika vituo mbalimbali nchini ili kusimamia ulinzi; kwa hiyo huenda ukawapo mpango wa kuwawezesha kupiga kura.

Kuondoa utata wa suala hili, ni vema Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na NEC wakatoa ufafanuzi ili kuwatoa hofu askari na wananchi ambao wangependa kuona Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na wa haki. Serikali inayoamini katika uwazi, bila shaka itatolea ufafanuzi jambo hili.
attachment.php
 
Kuna askari alikuja kijiwe cha kahawa akasema wao wameisha piga kura
 
Hii habari ni kweli, ndugu yangu ni askari ameniambia wamepewa agizo hilo na wakuu wao.
 
Spati picha,nivipi ukawa watafanikiwa kulinda kura za watanzania maana zipo za kutosha lakini watazilindaje?wajipange
 
Hata sisi boss wetu kada wa chadema ametuambia hapa kiwandani kwake tumpelekee kadi zetu
 
Hayo ni majibu tosha kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi NEC. Asipoteze muda kumsubiri Lowasa awaambie CCM wanaibaje kura. Aanzie hapo, na akikaa kimya kama suala hili ni la kweli basi tutajuwa ni mipango ya CCM na NEC.
 
Wakuu bao la mkono ndio hili?

Hili ni ombi langu kwenu tume. Mungu mwenyezi, muumba mbingu na nchi, amewaweka kutenda haki. Msipofanya hivyo, vilio vya watanzania vitafika juu mbinguni kwa Mungu, na mwenyewe atawaadhibu. Kumbuka, ipo siku kila utasimama mbele za Mungu na kutoa hesabu ya kila udhalimu na uovu. Especially, mtu unapokuwa mzee, ni bora kutenda haki, kwasababu siku si nyingi safari yako duniani itakwisha na utakwenda either kwenye moto wa milele kama ulidhulumu au mbinguni kama ulitenda haki. Mungu awasaidie, na kuwapa ujasiri.
 
Nimeshajiuliza sana wanakusanya vitambulisho ili wavifanyeje?
*Wadurufu vingine ?
*Waje wajue umepigie chama gani ?
*waviblock usiweze kupiga kura?
Wanavifanyia.nini?
 
Mzee mkubwa shaka ondoa Lubuva akijaribu kupindisha jambo lolote kwa faida ya ccm hukumu yake ni kufuata nyayo za Samuel Kivuitu wa kny.
 
Leo hii IGP akiwa Bukoba amekiri Jeshi hilo mkoani Pwani kukuhakiki shahada za askari Polisi ili kujua kama wote wamejiandikisha na ili kusaidia wale ambao hawajajiandikisha wajiandikishe.

IGP ametoa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajibu wa askari kushiriki uchaguzi na sababu nyingine ni askari wake kuwa katika maeneo tofauti tofauti ya kazi wakati zoezi la kujiandikisha likiwa linafanyika akimanisha askari hao kukosa fursa ya kujiandikisha.

Chanzo:ITV

Je,pamoja na sababu hizo,utaratibu huu ni sahihi kisheria?
 
Nae ata hajui sababu ila kwavile RIZWAN alimwambia fanya nalo likafanya
 
Hakuna kitu hapo sasa si wangekusanya majina ya polisi wasioandikishwa
 
Back
Top Bottom