Vitalis Maembe: Makonda shika adabu yako, Chuo cha Sanaa Bagamoyo si sawa na wasafi wa nguo

Uwasilishaji mbovu sana.
Hapana hii ni sanaa ya kumchana mtu kama unachana karatasi unapokata kata karatasi unfanya kwa mpangilio mzuri lakini kuchana karatasi ni ovyo ovyo na kwa kasi na hapa ninmuafaka kabisa kwa huyu DAB
 
Unawajuwa Tatu Nane? Tembea duniani kwenye matamasha makubwa ya muziki wanatambulika, huyo Diamond mpaka siku anakufa hatopanda hayo majukwaa ataishia kufanya show kwenye birthday party za Wabongo tu UK na USA.

Google kwanza Tatu nane huenda google watakupa msaada boya wewe.
Ahudhurie pia kazi za sisi tambala ndio ataelewa nn kinaendlea pale halafu akipata muda ajaribu kuongea na mwanamuziki wa regae jhiko man amuulize ametembelea nchi zipi na majukwa yake ni na kina nani na mwaka gani hajapata mualiko huko duniani tena waki "kiserikari" kwa hizo nchi akimaliza hiyo aje tena kutukana chuo cha sanaa bagamoyo
Hao wasafi huwezi walinganisha na hata THT
 
Hao wapiga vigelegele wa Lumumba hawajui watu mashuhuri katika sanaa za Tanzania. Hawajui chochote kuhusu "Sisi Tambala" "Dokta Ukwe zawose" au "Tinga tinga" na watanzania kibao wanaoishi Ulaya kwa kutegemea fedha zinazotokana na sanaa waliyojifunza Bagamoyo.
Ni kukosa elimu mkuu watu upeo wao mwisho instagram na Face book .
Hawaja shuhudia show za sisi tambala na tatu nane ughaibun hao
 
Vital Maembe yupo sahihi sana hasa ukilinganisha na alichokisema Mkuu wetu wa mkoa. Hiv ni sahihi kulinganisha taasisi kubwa dunian kama TASUBA, na kundi la wanamuziki la wasafi? Kufananisha walimu wa TASUBA, na waimbaji wa wasafi?

Mimi ninaufahamu mkubwa sana wa taasisi hii, toka ilivyokuwa inatambulika kwa jina la Chuo Cha Sanaa Bagamoyo, mpka sasa kuwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Kuna wasanii wengi wenye vipaji vyao, na huja pale kupata mafunzo juu ya vipaji vyao, kwan kuwa na kipaji ni suala lingine na kuwa na elimu ya kipaji chako, pia ni suala lingine.

Mkuu wetu wa mkoa, akitaka kujua watu wangapi wamezalishwa katika Taasisi hiyo, basi angekuja na kupata historia ya watu mashuhuli,( vip vyema kuwaanika hapa) waliopita katika kituo hicho. Pia kuna watu lukuki ambao ni waalimu wa sanaa katika vyuo vikuu vya ndani ya nchi na nje ya nchi pia, ebu angepata historia pale UDSM, kitivo cha FPA( fine and performing art) atapata kujua nani ni nani.
Kwa kumalizia tu, tusiwadharau walimu wetu wa hapa TASUBA, ndio miongoni mwa wadumisha mila na desturi za jamii yetu.
 
Kama jamii tumeathirika kwa kupenda vitu vyepesi vyepesi, twa ridhika kwa kucheza miziki ya kutayarishwa kwa kuiga uzungu, unaija na kudharau wanazuoni wetu wanaojitahidi kuutafiti na kuutunza utamaduni wetu!
 
Bora Asingejibu.. Hao Aliwataja wamelisaidia nini Taifa hili kama siyo kutafuna pesa za walipa kodi?? Wameshindwa hata kupeleka mawazo kwa Waziri wa Sanaa pale chuoni pawe na Studio ya kimataifa mapato yarudi selikalini?? Makonda Ana mapungufu mengi sana ila kwa Hili yuko sahihi...
Hao aliowataja wote anawajua yeye tu, niliyemtambua hapo ni Mzee Jangala peke yake.
 
"MAKONDA SHIKA ADABU YAKO" - MAEMBE .

AMUONYA AACHE KUFANANISHA CHUO CHA SANAA BAGAMOYO NA WASAFI.

Mwanamuziki Vitalis Maembe, amemjia juu Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda na kumtaka afute kauli yake na kuomba radhi kufuatia taarifa aliyoitoa kuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo hakijawahi kuzalisha mtu yeyote maarufu zaidi ya kutafuna fedha za mishahara wanazolipwa bila faida yeyote.

Makonda alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye viwanja vya Tandale wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa msanii Diamond Platinumz ambapo ilikwenda sambamba na msanii huyo kutoa misaada mbalimbali ya kijamii.

Kufuatia taarifa yake, Makonda alinukuliwa akisema kuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambapo kipo chini ya serikali, hakijawahi kutoa mtu yeyote mwenye tija kwa taifa hili zaidi ya kutumia fedha za serikali wanazolipwa, na kuongeza kuwa ni heri Wasanii wa kundi la Wasafi (WCB) wanafanya vitu vyenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla kuliko chuo hicho.

Kufuatia kauli hiyo, Maembe alionesha kukerwa na maneno ya Mkuu huyo na kutoa maelezo yafuatayo:

" Dogo Makonda, Shika Adabu yako!
Mnapotaka kuongelea vitu vilivyowazidi Umri mkasome kwanza au ulizeni wakubwa zenu wawaambie. Haya! Umezaliwa Mwanza Tarehe 15/02/1982. Chuo Cha Sanaa kimezaliwa Dar es salaam. Kimehamia Bagamoyo na kuanza Rasmi 1981. Serikali ya Tanzania ni kubwa kwako kwa Umri na kila kitu. Ongea lakini chunga ulimi wako!

"Mh. Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi wa BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) Ndugu Lebejo. Mkuu wa TaSUBa (Chuo Cha Sanaa Bagamoyo) Ndugu Makoye.
Mmemsikia Shoga yenu alichokisema kwenye sherehe ya shoga zake wasafi wa nguo?
Mwambieni kuwa yeye ni sehemu ya Serikali, kushindwa kwa Serikali ina maana naye kashindwa, asishabikie kushindwa bali ajirekebishe".

"Kama hajui au hamjui, Mwambieni,
Chuo cha Sanaa Bagamoyo ndiyo Chuo Sanaa pekee cha Umma Afrika kilichopata ithibati ya Ubora uliotukuka. Kwanini?
Chuo kinahistoria ya kutoa mchango mkubwa wa Mapinduzi ya Elimu ya Sanaa ya Afrika Duniani. Imetoa walimu wa sanaa wanao fundisha Vyuo vikuu vya Muziki ndani na nje ya nchi....Dr. Makoye, Dr Nyoni, Dr Kiagho, Dr. Chaya na wengine wengi. Ndiyo chuo pekee cha sanaa kilichowahi kukabidhiwa Zuria jekundu.

"Waigizaji kama Mzee Jangala na wengine wengi. Paul Ndunguru (Mchoraji wa vitabu vingi vya kufundishia Shule za msingi na Sekondari nchini) Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu, TaSUBA na hiyo BASATA,
Wataalamu wengi wa Media Tech ktk Vituo nyingi vya TV nchini wamesoma hapo.

"Mwakyembe, Lebejo na Makoye!

Japo sikumsikia Makonda lkn kama kaongea hivyo ni kweli...Tuwe na tabia ya kuukubali ukweli...Chuo cha sanaa kimemtoa nani ambaye amepeperusha bendera ya Tanzania km Diamond anavyofanya kwenye WCB ??
 
Nyinyi ni watumishi mlioaminiwa na Serikali, msinyamaze BOYA Kama huyo anapoitukana Serikali, nawapa siku 7 tuwasikie Mkikanusha au kumuunga mkono wazo lake kama kama 'Walimu wa TaSUBa wanapokea mishahara bure' Kwa sababu ya uzembe wenu na uwoga wenu ndiyo maana hata mafanikio madogo ya juhudi za Serikali hayathaminiwi." Alimalizia.

Maembe Vitali

Na hao ulowataja sisi vijana hatuwafahamu ni wa enzi hizo hatutaki mazoea, bali tunataka chuo kituonyeshe ya sasa...tusiongelee ya kale....sasa hivi kimemtoa nani akapeperusha bendera ??
 
Sasa Msanii na bado kashindwa kutumua lugha ya sanaa kuwasilisha ujumbe wake?

Sasa Chuo kimemsaidia nini hicho?
 
Bora Asingejibu.. Hao Aliwataja wamelisaidia nini Taifa hili kama siyo kutafuna pesa za walipa kodi?? Wameshindwa hata kupeleka mawazo kwa Waziri wa Sanaa pale chuoni pawe na Studio ya kimataifa mapato yarudi selikalini?? Makonda Ana mapungufu mengi sana ila kwa Hili yuko sahihi...
Change begins with you....
 
Back
Top Bottom