Kamati ya Bunge yapongeza TASUBA kwa kuzalisha wataalam wa sanaa na utamaduni

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
737
476
Kamati ya Kidumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti Mhe. Prof. Kitila Mkumbo imeipongeza Taasisi ya Sanaa na Utamaduni nchini (TaSUBa) kwa kufanya ukarabati na kununua vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi kama ilivyoelekezwa.

Machi 18, 2023, imetembela Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo kuona shughuli zinazotekelezwa na Taasisi hiyo, pamoja na Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/ 22.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Kitila Mkumbo ameyasema hayo wilayani Bagamoyo mara baada ya Kamati hiyo kutembelea Taasisi hiyo wilayani Bagamoyo, Machi 18, 2023, kukagua utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/ 22.

"Sekta ya Utamaduni na Sanaa inatoa ajira kwa watu wengi, ni vizuri tukaendelea kuwekeza na kuweka mazingira bora kwa Taasisi hii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kutosha na ununuzi wa vifaa vya kisasa ili wadau wetu wapate mafunzo bora ya kuendeleza vipaji vyao" Amesisitiza Mhe. Kitila.

Ameongeza kuwa ipo haja kwa Serikali kuiongezea Bajeti Taasisi hiyo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi pamoja na kuiongezea vifaa zaidi vya kujifunzia na kufundishia.

Kwa upande wao Wajumbe wa Kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo wametoa wito kwa wadau wa Sekta Binafsi hususani Wasanii na wanufaika wa kazi za sanaa waendelee kujitokeza kuchangia maendeleo ya taasisi hiyo kwa kujenga miundombinu na kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia badala ya kuiachia Serikali pekee.

Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameieleza Kamati hiyo kuwa Serikali inaeendelea kuboresha miundombinu ya Taasisi hiyo na kwamba inaendelea kuialika Sekta binafsi ishirikiane na Serikali katika kuiendeleza Taasisi hiyo.

IMG-20230319-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom