Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Je, unadhani maoni haya ni uonevu kwa Taasisi?

  • Ndio

    Votes: 1 20.0%
  • Hapana

    Votes: 4 80.0%

  • Total voters
    5
Kama la mihadarati lilitia watu ndani, kwa nini hili la kuwapa ujnga taifa lisifanywe vivyo hivyo?
 
Wanafanya nakosa ya makusudi ili wapewe tena tenda ya marekebisho... Incase kama ulikua hujui... I love this game
 
Nilimsikia waziri Ndalichako akisema waliofanya haya madudu watachukuliwa hatua na kwamba watachukua hatua kuwapata watu wenye ujuzi. Hiyo mimi naona ni tatizo lilelile. Kinachotakiwa ni kuacha tasnia iwe huru ili watu wapambanishwe kwenye uwanja huru; na sio kuhodhi mamlaka ya uandishi wa vitabu. State monopoly will generally not work.
Mhh umeshachunguza madhara ya kuwaachia akina nyambari nyangwine na wapambe wake uandishi wa vitabu vya kiada?
 
Mhh umeshachunguza madhara ya kuwaachia akina nyambari nyangwine na wapambe wake uandishi wa vitabu vya kiada?

Waachiwe tuu waandishi binafsi waandike, serikali ina mamlaka ya ukaguzi wa vitabu (EMAC). Vile vilivyokidhi vigezo na viwango vilivyowekwa na serikali waviteue vitumike shuleni. Kama mchapishaji atachapisha hataweza kupata ithibati ya kuonyesha vimepitiwa na serikali endapo havijakidhi viwango, hivyo hatoweza kuuza popote, simple!!
 
Mhh umeshachunguza madhara ya kuwaachia akina nyambari nyangwine na wapambe wake uandishi wa vitabu vya kiada?
Vinajulikana mheshimiwa. Ndio maana kinachotakiwa ni EMAC wafanye kazi yao. Wao wasimamie viwango. Huwezi kusema kwa kuwa bidhaa feki zinaingia nchini basi suluhisho ni kuvunja shirika la viwango (TBS).
 
Dah mkuu hongera sana kwa uchambuzi makini kama huu. Nadhani watajirekebisha.
Ni matumaini kuwa watasikia na yamkini mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi sahihi atafikiwa na ujumbe na kufanya lipasalo Usa-River. 🙂🙂🙂
 
Hizi ndizo mada makini ambazo zinatakiwa, nashangaa hata wachangiaji ni wachache ilhali hii ni mada ambayo inagusa maendeleo ya nchi yetu kielimu, dah ila watanzania sijui tumelogwa na nani.. Threads za ajabuajabu za kidaku na kimbeya ndo huwa zinachangiwa na watu wengi.
 
Daah!! Ndugu zangu hivi vitabu ishu sio typing errors sasa inakuaje mpaka sekondari na almost nusu ya michoro?? Ninachokiona hapa ni
1. Kutowajibika
2. Uzembe
3. Kutokuwa na uelewa juu ya kazi yao n.k
 
Kiswahili kimeshakuwa tatizo baada ya kuachwa kikiharibiwa na Wasanii pamoja na Watangazaji redioni. Hata wewe mleta mada unamakosa katika sentensi yako hii "nyingi ya hizi ni typing errors". Hatuna Kiswahili cha nyingi ya hizi. Na wewe umefanya makosa ya kutokana na kuyachukua maneno ya Kiingereza "Most of them". Ulitakiwa useme "makosa mengi ni ya uchapaji".

Sent from my HUAWEI Y511-U30 using JamiiForums mobile app
 
Daah!! Ndugu zangu hivi vitabu ishu sio typing errors sasa inakuaje mpaka sekondari na almost nusu ya michoro?? Ninachokiona hapa ni
1. Kutowajibika
2. Uzembe
3. Kutokuwa na uelewa juu ya kazi yao n.k
Nami naungana nawe kabisa Chuji. You are right.
 
Kiswahili kimeshakuwa tatizo baada ya kuachwa kikiharibiwa na Wasanii pamoja na Watangazaji redioni. Hata wewe mleta mada unamakosa katika sentensi yako hii "nyingi ya hizi ni typing errors". Hatuna Kiswahili cha nyingi ya hizi. Na wewe umefanya makosa ya kutokana na kuyachukua maneno ya Kiingereza "Most of them". Ulitakiwa useme "makosa mengi ni ya uchapaji".

Sent from my HUAWEI Y511-U30 using JamiiForums mobile app
Asante kwa sahihisho Shebbydo.
 
Back
Top Bottom