Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Je, unadhani maoni haya ni uonevu kwa Taasisi?

  • Ndio

    Votes: 1 20.0%
  • Hapana

    Votes: 4 80.0%

  • Total voters
    5

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
765
Kama ilivyokuwa kwenye post yangu iliyotangulia kuhusu kitabu cha Taasisi ya Elimu: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, ambacho ndio kimeandaliwa kusambazwa Tanzania nzima kama kitabu cha Kiada kwa ajili ya MAISHA ya wanafunzi na taifa, leo nitaendelea kubainisha makosa MACHACHE TU KATI YA MENGI ndani ya kitabu chao kingine: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili, ambacho ISBN yake kwenye uk i ni 978-9976-61-537-7 lakini kwenye uk ii ni 978-9976-61-535-7.

Ni maombi yangu kuwa watatokea wahusika watakaoweza kufanya kinachopaswa maana, kimsingi, vitabu hivi VINALETA MASHAKA MAKUBWA kwa hatma ya nchi yetu. Siamini kuwa suluhisho ni kuanza kuvitetea vitabu hivi.

Yafuatayo ni hayo makosa MACHACHE TU kati ya mengi kwenye: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili

1. Uk 8 pameandikwa: “Siku moja alinunua daftari nyingi …” ---- Je, wingi wa ‘daftari’ ni ‘daftari’? Kosa hili limerudiwa uk 23, 45, 64.
upload_2017-5-11_11-55-31.png
2. Uk 9 pameandikwa: “Angalia mchoro ufutao …”
upload_2017-5-11_11-55-52.png
3. Uk 19 pameandikwa: “Kujumlisha bila kubadili kwa wima” --- “kubadilini kwa wima” ndio kitu gani? Kilicho cha wima ni ‘kubadili’ au ni ‘kujumlisha’? Kosa hili limerudiwa uk 24, 40.
upload_2017-5-11_11-56-12.png
4. Uk 22 swali la 3 pameandikwa: “Wakaungana na wenzao 427 wa shule ya msingi mapambano.” --------- kwani japo ni Hesabu, ndio usizingatie matumizi sahihi ya herufi kubwa?
upload_2017-5-11_11-56-32.png
5. Uk 23 swali la 7 pameandikwa: “… mitihani yake ya darasa la kwanza na la pili?.” -------- sentensi inawezaje kuishia na alama ya kuuliza na nukta? Swali la 8 nalo hivyohivyo.
upload_2017-5-11_11-56-49.png
6. Uk 24 hatua ya kwanza inasema: “kuna makumi 1 …” lakini ya 2 inasema: “Jumlisha hiyo kumi 1…” -------- Kwa nini hapa useme “kumi 1”? Kosa hili limerudiwa uk 27, 40, 42, 43, 44.
upload_2017-5-11_11-57-8.png
7. Uk 26 kuna “Zoezi la 6” na wa 27 nako ni “Zoezi la 6”. Kosa la namna hii limerudiwa uk 28, 53, 66, 73, 74, 88, 93.
upload_2017-5-11_11-57-28.png
8. Uk 28 swali la 2 linaishia hivi: Shule hizo Jumla ya wanafunzi wangapi? --- wrong sentence.
upload_2017-5-11_11-57-44.png
9. Uk 29 wanasema: “Chati hii ina miraba ya ulalo na wima kama inavyooneshwa na mistari ya ulalo na wima” --- Hivyo, kuna miraba (square boxes) na mistari (arrows).

Lakini mtu atajiuliza:

MOJA: Mraba kama mraba mmoja unawezaje kuwa wa ulalo au wa wima?

MBILI: Aya ya pili inasema: “Ukichunguza mstari wa kwanza wa ulalo una namba 101, 102, 103, 104 na 105.” ----- kwa kuwa hapo juu umetofautisha kati ya mraba (square) na mstari (arrow), je, namba ziko kwenye mstari (arrow) au ziko kwenye mraba (square)?
upload_2017-5-11_11-58-2.png
10. Uk 38 swali la 1 linasema: “Kaka alikuwa na mayai 649, Akauza mayai 415. Alibaki na mayai mangapi? ----- “Alibaki”???

Swali la 6 linasema: “… alikuwa na midoli 888 akauza midoli 573. Alibakiwa na midoli mingapi? --------- hongera kwa kusema “Alibakiwa”. Lakini neno “midoli” ni Kiswahili sanifu?
upload_2017-5-11_11-58-22.png
11. Uk 54 wameandika: “Tunashikana mikono na kufanya duara.” ------- duara huwa linafanywa???
upload_2017-5-11_11-58-40.png
12. Uk 63 Zoezi la 1 limeshatimia na maswali yake na fremu yake, kisha nje ndio unaweka picha za sarafu na kusema: “Chunguza michoro ya sarafu zifuatazo.” Huoni kuwa hizo sarafu ndio zilitakiwa zianze, ndipo useme “Jibu maswali yafuatayo”?
upload_2017-5-11_11-58-56.png
Mtu mmoja akajibu akaniambia kuwa “nyingi ya hizi ni typing errors tu”. Japo si kweli, lakini hata kama zingekuwa ni typing errors peke yake, basi ndio mnataka kutuambia hamna mpango wa kuzisahihisha? Au mnamaanisha kuwa zinakubalika? Na kama mna mpango wa kuzisahihisha, mnaona ni sawa tu kutumia mabilioni ya fedha kuchapa upya vitabu ambavyo tayari mmeingiza makosa lukuki na vimeshazamisha fedha nyingi? Je, na hivi mnavyosambaza au mlivyosambaza mtavirudisha na kuvitupa?

Tunaponya taifa au tunaliangamiza?
 
.
 
Waziri ameahidi jana bungeni kuwa atawachukulia hatua waliohusika na uzembe huu.
Pamoja na kuwachukulia hatua hivyo vitabu wavichukue walikosambaza mashuleni viharibiwe visitumike. Eti walifanya semina mikoani kuhusu hivyo vitabu, daaaa serikali haiko makini jamani kwenye elimu. Vya sekondari ndio balaaa
 
Nakupongeza kwa uchanganuzi huu mwalimu,lakini vitabu vingi vina makosa ya aina zote.
Mbaya zaidi vitabu hivyo vina nembo ya EMAC (Educational Material Approval Committee).Yaani nao wamebariki huu ujinga wa kimaangamizi.
Niliwahi kuwatuhumu hawa EMAC kwa kuridhia vitabu vibovu kuingia mashuleni lakini naona mamlaka hazichukui hatua.
Ila ni bora kusema kuliko kukaa kimya.
 
Yaani vitafutwe kama mihadarati labda zibakie kopi tu makumbusho za kuonyesha tulifika wapi katika uzembe wetu wa pamoja kielimu. Hii ni zaidi ya vyeti feki-inaharibu msingi wa elimu kwa watoto na wajukuu wetu.
 
Nakupongeza kwa uchanganuzi huu mwalimu,lakini vitabu vingi vina makosa ya aina zote.
Mbaya zaidi vitabu hivyo vina nembo ya EMAC (Educational Material Approval Committee).Yaani nao wamebariki huu ujinga wa kimaangamizi.
Niliwahi kuwatuhumu hawa EMAC kwa kuridhia vitabu vibovu kuingia mashuleni lakini naona mamlaka hazichukui hatua.
Ila ni bora kusema kuliko kukaa kimya.
Nilimsikia waziri Ndalichako akisema waliofanya haya madudu watachukuliwa hatua na kwamba watachukua hatua kuwapata watu wenye ujuzi. Hiyo mimi naona ni tatizo lilelile. Kinachotakiwa ni kuacha tasnia iwe huru ili watu wapambanishwe kwenye uwanja huru; na sio kuhodhi mamlaka ya uandishi wa vitabu. State monopoly will generally not work.
 
Tatizo wanaandika vitabu ni walewale, mtu wa kiswahili anaandika kitabu mpaka cha hesabu, pia editors ni walewale wanashidwa kukosoa kwa kuhofia hawatapewa kazi tena
 
Nilimsikia waziri Ndalichako akisema waliofanya haya madudu watachukuliwa hatua na kwamba watachukua hatua kuwapata watu wenye ujuzi. Hiyo mimi naona ni tatizo lilelile. Kinachotakiwa ni kuacha tasnia iwe huru ili watu wapambanishwe kwenye uwanja huru; na sio kuhodhi mamlaka ya uandishi wa vitabu. State monopoly will generally not work.

ADHABU ZA WALIOHARIBU VITABU VYA TAASISI YA ELIMU
IANZE NA WAZIRI WA ELIMU - J. NDALICHAKO

Ina maana waziri Ndalichako hakujua kilichoandikwa ndani ya hivyo vitabu vibovu? Ndalichako amekuwa akizunguka na wakuza mitaala mikoani akifungua/kufunga semina elekezi kwa waalimu namna ya kutumia vitabu hivyo vibovu, iweje apongezwe? Angekuwa na nia nzuri na elimu ya watoto wa kitanzania angekataza wasiendeshe hizo semina kwa sababu ni upotevu wa fedha za walipa kodi. Kushindwa kufanya hivyo ina maana kuwa HAFAI kuwepo kwenye nafasi ya uwaziri wa elimu. Waziri Ndalichako linda heshima yako kwa kujiuzulu tuu. Kama sivyo mamlaka yake ya uteuzi iangalie hili na ampangie kazi nyingine japo hatushurutishi kufanya hivyo.
 
Mawaziri wetu hasa ktk elimu ni wababaishaji,kama wewe waziri unalalamika huku una mamlaka ujue wewe ni jipu.
 
Kama ilivyokuwa kwenye post yangu iliyotangulia kuhusu kitabu cha Taasisi ya Elimu: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, ambacho ndio kimeandaliwa kusambazwa Tanzania nzima kama kitabu cha Kiada kwa ajili ya MAISHA ya wanafunzi na taifa, leo nitaendelea kubainisha makosa MACHACHE TU KATI YA MENGI ndani ya kitabu chao kingine: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili, ambacho ISBN yake kwenye uk i ni 978-9976-61-537-7 lakini kwenye uk ii ni 978-9976-61-535-7.

Ni maombi yangu kuwa watatokea wahusika watakaoweza kufanya kinachopaswa maana, kimsingi, vitabu hivi VINALETA MASHAKA MAKUBWA kwa hatma ya nchi yetu. Siamini kuwa suluhisho ni kuanza kuvitetea vitabu hivi.

Yafuatayo ni hayo makosa MACHACHE TU kati ya mengi kwenye: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili

1. Uk 8 pameandikwa: “Siku moja alinunua daftari nyingi …” ---- Je, wingi wa ‘daftari’ ni ‘daftari’? Kosa hili limerudiwa uk 23, 45, 64.
2. Uk 9 pameandikwa: “Angalia mchoro ufutao …”
3. Uk 19 pameandikwa: “Kujumlisha bila kubadili kwa wima” --- “kubadilini kwa wima” ndio kitu gani? Kilicho cha wima ni ‘kubadili’ au ni ‘kujumlisha’? Kosa hili limerudiwa uk 24, 40.
4. Uk 22 swali la 3 pameandikwa: “Wakaungana na wenzao 427 wa shule ya msingi mapambano.” --------- kwani japo ni Hesabu, ndio usizingatie matumizi sahihi ya herufi kubwa?
5. Uk 23 swali la 7 pameandikwa: “… mitihani yake ya darasa la kwanza na la pili?.” -------- sentensi inawezaje kuishia na alama ya kuuliza na nukta? Swali la 8 nalo hivyohivyo.
6. Uk 24 hatua ya kwanza inasema: “kuna makumi 1 …” lakini ya 2 inasema: “Jumlisha hiyo kumi 1…” -------- Kwa nini hapa useme “kumi 1”? Kosa hili limerudiwa uk 27, 40, 42, 43, 44.
7. Uk 26 kuna “Zoezi la 6” na wa 27 nako ni “Zoezi la 6”. Kosa la namna hii limerudiwa uk 28, 53, 66, 73, 74, 88, 93.
8. Uk 28 swali la 2 linaishia hivi: Shule hizo Jumla ya wanafunzi wangapi? --- wrong sentence.
9. Uk 29 wanasema: “Chati hii ina miraba ya ulalo na wima kama inavyooneshwa na mistari ya ulalo na wima” --- Hivyo, kuna miraba (square boxes) na mistari (arrows).

Lakini mtu atajiuliza:

MOJA: Mraba kama mraba mmoja unawezaje kuwa wa ulalo au wa wima?

MBILI: Aya ya pili inasema: “Ukichunguza mstari wa kwanza wa ulalo una namba 101, 102, 103, 104 na 105.” ----- kwa kuwa hapo juu umetofautisha kati ya mraba (square) na mstari (arrow), je, namba ziko kwenye mstari (arrow) au ziko kwenye mraba (square)?
10. Uk 38 swali la 1 linasema: “Kaka alikuwa na mayai 649, Akauza mayai 415. Alibaki na mayai mangapi? ----- “Alibaki”???

Swali la 6 linasema: “… alikuwa na midoli 888 akauza midoli 573. Alibakiwa na midoli mingapi? --------- hongera kwa kusema “Alibakiwa”. Lakini neno “midoli” ni Kiswahili sanifu?
11. Uk 54 wameandika: “Tunashikana mikono na kufanya duara.” ------- duara huwa linafanywa???
12. Uk 63 Zoezi la 1 limeshatimia na maswali yake na fremu yake, kisha nje ndio unaweka picha za sarafu na kusema: “Chunguza michoro ya sarafu zifuatazo.” Huoni kuwa hizo sarafu ndio zilitakiwa zianze, ndipo useme “Jibu maswali yafuatayo”?
Mtu mmoja akajibu akaniambia kuwa “nyingi ya hizi ni typing errors tu”. Japo si kweli, lakini hata kama zingekuwa ni typing errors peke yake, basi ndio mnataka kutuambia hamna mpango wa kuzisahihisha? Au mnamaanisha kuwa zinakubalika? Na kama mna mpango wa kuzisahihisha, mnaona ni sawa tu kutumia mabilioni ya fedha kuchapa upya vitabu ambavyo tayari mmeingiza makosa lukuki na vimeshazamisha fedha nyingi? Je, na hivi mnavyosambaza au mlivyosambaza mtavirudisha na kuvitupa?

Tunaponya taifa au tunaliangamiza?
Hata kama ni typing error hatukatai je hawa emac wanagonga mhuri ktk kitabu baada ya kukihariri au bila kuhaririwa?.
Tusipelekwe nje ya mada.
 
Back
Top Bottom